Dkt. Peter Maiga Nyanja aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba na Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe leo tarehe13 Machi 2024 amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Bw.Isaya Mugishagwe Mbenje.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Muleba, mbele ya Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Magongo Justus,Katibu Tawala wa Wilaya Mhe. Benjamini Mwikasyege pamoja na Wataalam wa Halmashauri(CMT).
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Magongo Justus amemkaribisha na kumuahidi kumpa ushirikiano wa kutosha kwa kufanya kazi kwa umoja, mshikamano na kwa mafanikio ya Wilaya yetu.
Aidha Mhe. Magongo ameendelea kusema palipo na umoja ndio sehemu pekee ambapo mafanikio hutokea hivyo kwa umoja wetu tukiunganisha nguvu, tukawa na sauti moja vita ya maendeleo tutaishinda.
Kwa upande wake Mhe.Benjamini Mwikasyege Katibu tawala wa Wilaya ameeleza bayana kuwa Halmashauri ya Muleba ni kubwa hivyo kazi ya ziada inahitajika hasa katika ufuatiliaji na ukamilishaji wa Miradi ya Maendeleo.
Akizungumza wakati wa Makabidhiano Dkt.Peter Nyanja ameshukushuru Uongozi wa Wilaya pamoja na Watumishi wote Kwa ushirikiano waliomuonyesha na kuwaomba kutoa Ushirikiano zaidi kwa Mkurugenzi mpya ili kuhakikisha Miradi yote ya kimkakati inakamilika.
Aidha,Dkt. Nyanja amesema kuwa Miradi hiyo ni ujenzi wa Soko la Kariakoo pamoja na Miradi mingine ya Kimkakati ili kufikia lengo la kukusanya bilioni 10 za mapato ya ndani kwa mwaka huu wa fedha.
Akikabidhiwa Ofisi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Bw. Isaya Mbenje amewataka watumishi kushirikiana kwa pamoja katika kusimamia na kukamilisha miradi yote ya maendeleo ambayo imeletwa kwa wananchi ili kukuza uchumi wa Wilaya na Taifa kwa ujumla.
Nae,Bi.Christina Akyoo aliekuwa Kaimu Mkurugenzi alitumia muda huo pia kuishukuru Baraza la Madiwani wataalamu pamoja na Kamati Usalama kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote wakati akikaimu Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.
Imeandaliwa na kutolewa na;
Eusebius J.Kiluwa
Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa