Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Kemirembe Rwota ametoa mda wa miezi mitatu kwa mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji Kyamyorwa uliopo katika Kata ya Kasharunga Wilayani Muleba kukamirisha utekelezaji wa mradi huo ili wananchi waweze kupata huduma ya maji.
Akizungumza alipotembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo Kaimu Mkuu wa Wilaya amesema kuwa kwa fedha ipo ya kutekeleza na kukamilisha mradi huo hakuna sababu yeyote ya kuongeza mda mrefu Wa kukamilisha mradi huo.
"Watu wa Kyamyorwa wanataka maji haraka iwezekanavyo fedha ipo kinachotakiwa sasa ni maji hivyo tunawaongeza miezi mitati tu ili mwezi wa tatu mama zetu na baba zetu wanaoishi eneo la Kyamyorwa waweze kupata maji na hili tunakwenda kulisimamia na tutahakikisha kazi inafanyika usiku na mchana ili mwezi wa tatu maji yaweze kupatikana" amesema Mhe. Kemirembe Rwota.
Aidha, Amewasihi wananchi kuhakikisha wanailinda miradi ya maji kwa kuhakikisha wanakuwa wazalendo ili miradi hiyo iweze kudumu na kutumika kwa mda mrefu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
"Tunatakiwa kuwa wazalendo na kuwa na wivu na miradi inayoletwa kwenye maeneo yetu sisi ndio tuwe wa kwanza kuilinda sio tuanze kuiba na kuharibu miradi hii" amesema Mhe. Kemirembe Rwota.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kasharunga Mhe. Theobadi Kulandebe amemuomba Kaimu Mkuu wa Wilaya kwa wananchi waliopo karibia na eneo la tenki la maji lilipojengwa kuwekwa kwenye mpango wa kunufaika na huduma hiyo ya maji.
Aswida Athuman Mkazi wa Kyamyorwa ameeleza kuwa kupitia mradi huo utaweza kuwasaidia kuondokana na changamoto ya maji ambapo amesema kuwa hapo awali walikuwa wanategemea maji ya visima maji ambayo msimu wa kiangazi yalikuwa yanakauka lakini kupitia mradi huu wanaimani wataweza kuondokana na changamoto hizo.
Naye Ester Nyanda ambaye pia ni mkazi wa Kyamyorwa amesema kuwa upatikanaji wa maji katika eneo hilo kwani hata maji yaliyopatikana kwa kuchimba yalikuwa hayatoshi kumudu mahitaji yao.
Mradi wa maji Kyamyorwa unatekelezwa kwa kiasi cha Tsh Bilioni 3.2 Kwa fedha za PFR na mpaka sasa mkandarasi anayetekeleza mradi huo amelipwa kiasi cha Tsh. Bilioni 1.2
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa