Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, imenunua Fiber Patrol Boat (Horse Power 40) yenye thamani ya Shilingi Million 53.1 pamoja na Gari Toyota Hilux lenye thamani ya Shilingi milioni 93 fedha iliyotokana na makusanyo ya Mapato ya Ndani kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Katika mwaka wa fedha 2016/2017, Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ilikisia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 2.5 fedha za makusanyo ya ndani na hadi kufikia tarehe 30/06/2017, Halmashauri ilikuwa imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 2.6 sawa na asilimia 106 na kuvuka lengo na ziada ya shilingi milioni 141,931,455.63 ya makisio ya mwaka.
"Halmashauri imeona ni vema kununua vifaa (gari na boti) ambavyo vitasaidia na kuongeza kasi zaidi ya ukusanyaji wa mapato. Naamini vyombo hivi vitarahisisha kufika katika maeneo ya kukusanyia mapato kwa wakati na kuwezesha kukusanya kama ilivyokusudiwa." alieleza Ndg. Emmanuel Sherembi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Boti hii ina uwezo wa kubeba abiria 12 na mizigo yenye uzito wa tani moja ambayo pia itasaidia katika doria za udhibiti wa uvuvi haramu katika mipaka ya ziwa Viktoria wilayani Muleba. Pia ina vifaa vya usalama vikiwemo maboya 3 yenye kuhimili watu 4 kila moja na makoti ya kuogelea (Life Jacket) 12. Aidha boti hiyo ina injini ya ziada yenye (horse Power) 40 ambayo itatumika pale inapotokea dharura injini iliyopo kushindwa kufanya kazi au kupata itilafu.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa