Akizungumza katika ziara hiyo alipotembelea na kukagua shughuli zinazofanyika katika Mwalo huo Waziri Mkuu amesema kuwa kukamilika kwa Gati litawasaidia wananchi kuendesha vyema shughuli zao za uvuvi, kurahisisha shughuli za usafirishaji pamoja na kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo kujiingizia kipato.
"Walipokuwa wamejenga mala ya kwanza walikuwa wamekadilia kidogo maji yalikuwa yanafunika hili Gati na kwa hiyo mvua zikiwa nyingi tutashindwa kusafiri kutoka hapa Magarini kwenda kwenye visiwa vingine na kwahiyo natoa maelekezo Mamlaka ya Bandari watenge fedha haraka waje hapa wamalize kujenga eneo hili" amesema Mhe. Kassim Majaliwa.
Lakini pia ameiagiza Halmashauri kwa kushirikiana na Mamlaka ya Bandari kukaa kikao cha pamoja kujadili na kuweka bei sawa katika maeneo ya kuhifadhia mizigo ili kuweza kuwaondolea changamoto wananchi ya kushindwa kuamua ni wapi wanaweza kuhifadhi mizigo yao pamoja na kuisaidia Halmashauri na Mamlaka ya Bandari kuingiza Mapato yanayotokana na Maghala ya kuhifadhia mizigo.
Sambamba na hayo ameagiza kuongezwa kituo cha TANAPA katika mwalo wa Magarini ili hata watalii wanaoenda Kutalii Katika hifadhi ya Rubondo waweze kupita katika Bandari ya Magarini ambapo amemuagiza kamishna wa ardhi Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri wafike eneo la Magarini na kukagua eneo hilo na fursa zake ili kuweza kupata eneo la kuweka kituo cha TANAPA.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa