Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (MST) Salum M. Kijuu amezindua wiki ya maji Ki mkoa wilayani Muleba katika kijiji Ruhanga, kata ya Ruhanga na kuwasihi wananchi kutunza na kuhifadhi vyanzo vya maji kwa manufaa ya taifa letu.
Akizindua maadhimisho hayo, Meja Jenerali (MST) Salum M. Kijuu, amewasihi wananchi kusimamia ipasavyo miradi iliyojengwa na Serikali kwani imegharimu kiwango kikubwa cha fedha hivyo ni vema wananchi wakaipokea na kuitunza kama mali zao.
"Serikali imetumia fedha nyingi sana katika kuhakikisha wananchi wake wanasogezewa karibu huduma ya maji ili kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji hivyo ni jukumu letu wananchi kuitunza na kuisimamia ipasavyo miradi hii" alieleza Meja Jenerali (MST) Salum Kijuu.
Maadhimisho haya huadhimishwa kitaifa kila mwakakuanzia tarehe 16-22 Machi.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa