Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Kaigara Dr. Amlan Kite amewataja wazee kuwa ni miongoni mwa watu
wanaopewa kipaumbele katika kupatiwa huduma bora za afya kwenye siku ya wiki ya utumishi wa umma
alipotembelewa na wakaguzi kutoka Halmashauri ya Wilaya Muleba.
Dr. Amlan Kite amesema kwamba katika kuhakikisha wazeee wanapatiwa huduma iliyo bora wameweza
kufanikisha zoezi la kuweka bango nje ya mlango wa kuingilia kituoni hapo kwa kuandika "MPISHE MZEE
APATE HUDUMA" maneno ambayo yameandikwa kwenye bango ili kuonyesha ni kwa jinsi gani kituo cha
Kaigara kinatekeleza jukumu la kuhakikisha kwamba mzee anapewa kipaumbele katika kupatiwa huduma
iliyobora ya kiafya.
"Ukishaingia pale mapokezi kuna kibao ambacho kimeandikwa "MPISHE MZEE APATE HUDUMA",
tunachokifanya asubuhi mtu ambaye yupo kwenye dirisha la huduma kwa wateja anaanza kwanza na wazee
kwa kuangalia kama kuna mgonjwa mwenye uhitaji wa huduma ya haraka kama asipokuwepo tunaanza na
wazee" Ameeleza Dr. Amlan Kite.
Lakini pia ameweza kuongeza kwa kueleza ni kwa namna gani wazee wanapata huduma ya dawa ambapo
ameeleza kuwa wazee wapo kwenye makundi ya wanaolipa na wasio lipia kwa kuzitaja sifa za mzee ambaye
hatatakiwa kulipia huduma.
"Wazee tumewaweka kwenye makundi kuna makundi ambayo wazee wanalipia na wasiolipia kwa wasio lipia ili
uweze kuwekwa katika kundi la wazee ambao hawalipii kuna vigezo huwa tunavizingatia kigezo cha kwanza
anatakiwa kuwa na umri wa miaka kuanzia sitini(60), lakini kigezo cha pili mzee asiwe na mtoto yeyote mwenye
uwezo wa kumsaidia kimatibabu na kigezo cha tatu mzee asiwe na aina yeyote ya kipato tukishajiridhisha kuwa
mzee ana vigezo hivi mzee atatakiwa kwenda kwa mwenyekiti kupatiwa baarua na huduma zake zitakuwa ziko
huru kabisa". Ameeleza Dr. Amlan Kite.
Kwa upande wa bima ya afya Dr. Amlan Kite ameeleza kuwa kituo cha afya Kaigara kinatoa huduma ya bima
ya aina mbili ya kwanza ni CHIF iliyoboreshwa na NHIF, na kuongeza kuwa wanajitahidi kuwa wanatoa dawa
kwa kuhakikisha kuwa mteja mwenye bima ya afya anapatiwa huduma bora.
Kwa upande mwingine Dr. Amlan Kite ameweza kuzungumzia suala la usalama katika kituo cha afya Kaigara
Dr. Amlan amesema kuwa kituo hakina uzio ila kituo kina walinzi wawili ambao wanaingia kwa zamu usiku
ili kuhakikisha usalama upo kituoni hapo.
"Hatuna uzio kwa sasa lakini bado nafikiri kwa pesa illiyopo haitatosha kumalizia lakini mbali na uzio tunao
walinzi ambao hulinda usiku kwa hiyo kwa suala la usalama tunatumia walinzi". amemalizia Dr. Amlan Kite.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa