Katika kikao cha maridhiano baina ya Mkoa wa Kagera na Mkoa wa Geita kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba kujadili namna ya kuziondoa sintofahamu kuhusiana na masoko ya dagaa kamati za usalama za mikoa yote miwili pamoja na kamati ya usalama ya wilaya ya Chato na wilaya ya Muleba zimefanikiwa kuliondoa tatizo hilo.
Akizungumza katika kikao hicho mkuu wa Mkoa wa. Geita Mhe. Rosemary Seyamule amesema kuwa wafanyabiashara wanaruhusiwa kwenda kuuza dagaa mahari popote baada ya kulipa ushuru katika Halmashauri husika.
"Kama umepata dagaa katika Halmashauri ya Muleba unatakiwa kulipa ushuru wote ambao unahusika pale na baada ya hapo unaruhusiwa kwenda kuuza katika soko ambalo ungependa kulitumia" Amesema Mhe. Rosemary Seyamule.
Aidha, amesema kuwa kama ikitokea kuwa kuna changamoto yeyote ambayo iko kinyume na jambo hilo basi yatatolewa mawasiliano ya simu ambapo amewaagiza kufanya kwa viongozi husika wakiwemo Mkuu wa wilaya, Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi na hata viongozi wa ngazi za wizara na ngazi za chini kama watendaji wa kata na vijiji.
Lakini pia ameongeza kwa kusema kuwa zitaundwa kamati zitakazohusisha wataalamu kutoka Mkoa wa Kagera na Mkoa wa Geita ambao wataalamu hao watafanya kazi kwa haraka kuweza kutatua changamoto nyingine zinazoendelea kukwamisha wafanyabiashara kufanya biashara kwa amani na utulivu lakini pia kufanya biashara ziweze kuimalika kwa kukusanya mapato sahihi.
"Kamati hizo zitaundwa kupitia makatibu tawala wa mikoa hii miwili na kamati hiyo itaanza kufanya kazi haraka na itatoa matokeo ya kwanza ndani ya mwezi huu wa kwanza kabla ya tarehe 31 mwezi wa kwanza" amesema Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Sambamba na hayo amesisitiza kuwa Mikoa yote miwili pamoja na wilaya zote mbili zitaendelea na vikao vya ujilani mwema kila baada ya miezi mitatu ili kuweza kubaini kama kuna changamoto ambapo amesema kuwa kamati hizo zitakazo undwa zitakuwa endelevu ambazo zitaundwa kusimamia masoko kamati zile zitakuwa zinaleta taarifa hizo baada ya Tarifa ya mwezi wa kwanza kila baada ya miezi mitatu.
Hakuishia hapo akaongeza kwa kutoa wito kwa wafanyabiashara wote wadagaa na wananchi wote wadagaa na wananchi wote Kama Watanzania kuwa wanaowajibu kabisa wa kuhakikisha wanafanya kazi kwa uadilifu ikiwa ni pamoja na kulipa kodi zote za serikali kama inavyotakiwa kwa kuhakikisha wanafuata taratibu zote ambazo zimewekwa na Serikali.
Naye Katibu tawala wa Mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamzora amesema kuwa Soko la Magarini ni soko rasmi la Kimataifa la mazao ya uvuvi na soko hilo limeruhusiwa tayari na wizara ya mifugo na uvuvi na tayari wataalamu wa kudhibiti ubora na kutoa vibari vyote tayari wameshafika.
"Tayari wizara imeshatupa wataalamu tunaishukuru sana wizara na kwa mantiki hiyo masoko yote ambayo ni rasmi yanaruhusiwa kufanya kazi likiwepo na hili soko la Magarini sisi zaidi Mkoa wa Kagera na kwa niaba ya wakazi wote wa wilaya ya Muleba na Kagera kwa ujumla kwakweli tunaishukuru sana Serikali" ameendelea kusema.
"Tunahaidi kwamba maelekezo yote ya kuzingatia ubora kuboresha miundombinu na mpaka sasa hivi tayari mawakala wa Benki wanamalizia hatua za kufungua biashara pale Magarini kwahiyo tunawakaribisha wafanyabiashara kokote pale walipo kutumia hili soko na mengine yataendelea kufunguliwa kadri utaratibu wa wizara utakavyoendelea kutekelezwa" amesema Prof. Faustin Kamzora.
Imeandaliwa na kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa