Januari,2024 kiasi Cha shilingi Bil.1 kinatarajiwa kutolewa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuendeleza ujenzi wa majengo mengine mapya ya Hospitali ya Wilaya ya Muleba ambayo kwa sasa ukamilishaji wa ujenzi wa baadhi ya majengo unaendlea.
Akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Muleba Mhe.Mohamed Mchengerwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amesema kuwa Serikali itatoa Kiasi Cha Shilingi Bil.1 ilikuongeza majengo mengine mapya katika Hospitali ya Wilaya ili kuwezesha huduma bora kwa Wananchi wa Wilaya ya Muleba.
"Wabunge wameomba sana kuhusiana na hili swala lakini nimelipeleka kwa Waziri Mkuu hivyo nimemwagiza Katibu Mkuu kuwa ifikapo mwezi Januari, 2024 Mhe.Rais amesema ataleta kiasi Cha Tshs Bil.1 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mengine mapya ya Hospitali ya Wilaya."
Aidha Mhe.Mchengerwa amesema Serikali itaongeza vituo vya Afya vipya viwili ambavyo vitajengwa katika Wilaya ya Muleba huku kimoja kikitarajiwa kujengwa katika Jimbo la Muleba Kusini na kingine ambacho kinatarajiwa kujengwa katika Jimbo la Muleba Kaskazini.
"Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan anawapenda sana amesema atawaongezea kiasi kingine Cha fedha ili Kujenga vituo vya Afya viwili ambavyo vitajegwa katikaJimbo la Muleba Kaskazini na Jimbo la Muleba Kusini, lakini pia kwa Jografia ya Muleba nimemwagiza Katibu Mkuu kutafuta fedha nyingine ili tuongeze zahanati nyingine katika Wilaya ya Muleba na Wabunge wenu watachagua zijengwe wapi"
Sambamba na hilo Mhe.Mchengerwa ameongeza kuwa Serikali inatarajia kuleta Magari mawili ya wagonjwa yaani(Ambulance) na Boti ya kisasa (Fiber Boat) yakubebea wagonjwa(ambulance) ambazo zitasaidia kuboresha huduma ya Afya katika Jimbo la Muleba Kaskazini na Jimbo la Muleba Kusini.
"Mhe.Rais ameridhia na ameniambia ataleta gari mbili za wagonjwa na gari moja itapelekwa Muleba Kusini na gari Nyingne itapelekwa Muleba Kaskazini,lakini pia kule kwa kaka yangu Mwijage Mhe.Rais amesema ataleta Boti ya wagonjwa(ambulance) inayo kimbia kwa kasi zaidi kwenye maji"
Kwa upande wao wabunge wa Muleba(Kusini na Kaskazini) Mhe.Charles Mwijage na Mhe.Oscar Kikoyo walitumia muda huo kumshukuru na kumpongeza Mhe.Rais pamoja na Mhe.Mchengerwa kwa kazi kubwa wanayoifanya kwani Wilaya ya Muleba imeletewa Miradi Mingi Ikiwa ni pamoja na Miradi ya Afya, Shule, Maji pamoja na Miradi ya Barabara inayotekelezwa na Tarura.
Imetolewa na;
Kaimu Mkuu Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa