Mkuu wa wilaya ya Muleba, Mhe. Toba Nguvila amezindua rasmi kambi ya vijana wa Chama cha Mapinduzi waliojitolea kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ikiwa ni mkakati wa kuimarisha benki za matofari kwa kila kata, wilayani Muleba.
Akizindua rasmi kambi hiyo ya ufyatuaji wa matofali Mkuu wa wilaya amewashukuru vijana hao kwa kujitolea kwao kushiriki katika shughuli za maendeleo
"Nawapongeza sana kwa utayari wenu wa kujitoakuja Kushiriki katika zoezi hili ambalo tutalitekeleza katika kata zote 43 za wilaya ya Muleba kwa kujitoa kwenu nami nitahakikisha kuwapa kipaumbele kwa fursa zitakazokuja wilayani kwetu ikiwemo utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta kama sehemu ya motisha" ameeleza Mkuu wa Wilaya.
Aidha, ametoa salamu za waheshimiwa wabunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini Mhe. Charles Mwijage na Jimbo la Muleba Kusini Mhe. Dr. Oscar Kikoyo kuwa wapo pamoja nao katika kutekeleza mpango wa benki ya matofali na wanawashukuru sana kwa kujitoa kwao.
Kambi hiyo inaundwa na vijana wa Chama cha Mapinduzi wapatao 70 wanaume 55 na wanawake 15 kutoka katika kata za Ngenge, Ibuga, Muleba, Bureza na Kibanga.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Comred Mtwaafu Kantangayo ameeeleza kuwa kwa siku mbili wanaweza kufyatua jumla ya tofari 12,668.
Uzinduzi huu umefanyika katika kijiji cha Kibanga, kata ya Kibanga leo tarehe 10.08.2021.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Halmashauri ya wilaya ya Muleba
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa