Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Muleba ikiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya Ndg. Greyson Mwengu imefanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya pamoja na jengo la dharula katika Kituo cha Afya Kaigara na kuagiza Kukamilika kwa ujenzi huo ndani ya mwezi mmoja.
Akizungumza katika ziara hiyo Katibu Tawala wa Wilaya ya Muleba Ndg. Greyson Mwengu amesisitiza kukamilika kwa majengo ya Hospitali ya Wilaya ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.
"Kwa kipindi cha mwezi mmoja kazi iwe imekamilika kwa sababu fedha ipo na vifaa vipo hivyo ni vyema kazi ikakamilika kwa wakati" amesema Ndg. Greyson Mwengu
amesema kuwa kwa upungufu wa fedha za kumalizia katika ujenzi wa jengo la dharula tayari wataalamu wameshaomba fedha Halmashauri za kumalizia jengo hilo.
NayeMgangaMfawidhiwaKituochaAfyaKaigaraDr.AmranKiteameelezakuwaKituochaAfyaKaigarakilipokeakiasichaTsh.Milioni300kwaajiliyaujenziwajengoladharulampakasasamradiwaujenziwajengohiloupokatikahatuayaza ukamilishaji
Kwa upande wake Katibu wa Afya Ndg. Auxsilius Mathew Amesema kuwa ujenzi ulianza rasmi tarehe 27, Mei 2022 na ulitegemewa kukamilika 27, Julai 2022 na mpaka sasa jengo la wagonjwa wa nje limefika katika hatua ya uezekaji na jengo la maabara lipo katika hatua ya ukamilishaji, hadi sasa mradi umetumia jumla ya shilingi 452 na kiasi kilichobaki ni shilingi milioni 48 na kazi bado inaendelea.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa