Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila amewagiza Wakala wa usambazaji wa maji vijijini (RUWASA) endapo ikifika jumapili ya wiki hii Mkandarasi hajaanza kazi asimamishwe kazi ya kutekeleza mradi wa maji wa Buganguzi wilayani Muleba.
Akizungumza katika ziara hiyo ya kukagua miradi ya maji ya RUWASA aliyoifanya katika mradi wa maji wa Buganguzi uliopo kata ya Buganguzi ambao unatarajia kuvihudumia vijiji vinne amuomba mkandarasi kuanza kazi haraka baada ya kukuta ujenzi wa kisima haujaanza katika mradi huo.
"Kama mkandarasi hata hana pesa ya kuanza kujenga mradi hauna inaonyesha ambavyo hujajipanga kutekereza mradi huu naagiza ikifika jumapili hujaanza kazi ufukuzwe atafutwe mkandarasi mwingine wananchi hawawezi kuwa wanapata shida ya maji wakati mkandarasi hutekelezi kazi yako" amesema Mhe. Toba Nguvila.
Katika ziara hiyo pia ameutembelea mradi wa maji wa Buramula uliopo katika kijiji cha Buramula Kata ya Kamachumu na kukagua chanzo cha maji pamoja na maendeleo ya ujenzi wa visima vya maji vya mradi huo.
Akizungumza katika mradi huo ameuagiza uongozi wa eneo hilo kupanda miti mingi katika eneo hilo ili kutunza chanzo cha maji cha mradi huo wa maji ili kuweza kusaidia upatikanaji wa maji mengi ambayo yataweza kutumiwa na watu wa Kamachumu
Kwa upande wake diwani wa Kata hiyo Mhe. Reodigadi Peter Chonde ametoa shukrani kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa mradi wa maji katika kata hiyo na kuhaidi kuhakikisha wanakitunza chanzo cha Maji cha Buramula.
Lakini pia Mkuu wa wilaya ameutembelea mradi wa maji wa Kagoma na,kukagua ujenzi wa kisima pamoja na chanzo cha maji cha mradi huo.
Akizungumza katika mradi huo Mkuu wa wilaya amemuagiza Mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha anamaliza mapema mradi huo na kumueleza kuwa kama akifanya vizuri na kumaliza haraka mradi huo atakuwa na nafasi ya kupewa kazi katika miradi mingine.
Imeandaliwa na Kutolewa na;
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa