HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.) WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA UZINDUZI WA MFUMO, KUPANGA MIPANGO, KUANDAA BAJETI NA KUTOLEA TAARIFA (PLANREP) NA MFUMO WA MALIPO NA KUTOA TAARIFA ZA FEDHA ZA VITUO VYA KUTOA HUDUMA TAREHE 05 SEPTEMBA, 2017 - DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Mhe. George Simbachawene, (Mb.);
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Mhe. Jenista Mhagama, (Mb.);
Waziri wa Fedha na Mipango - Mhe. Dkt. Philip Mpango, (Mb.);
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto - Mhe. Ummy Mwalimu, (Mb.);
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia - Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, (Mb.);
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma - Mhe. Jordan Rugimbana;
Makatibu Wakuu mliopo;
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia - Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, (Mb.);
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma - Mhe. Jordan Rugimbana;
Makatibu Wakuu mliopo;
Makatibu Tawala - Mkoa wa Dodoma na Manyara;
Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania - Bi. Inmi Patterson;
Mkurugenzi wa USAID Tanzania - Bw. Andrew Karas;
Mkurugenzi wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma - Dkt. Emmanuel Malangalila;
Kiongozi wa Mradi wa Kuimarisha Huduma za Afya - Prof. M. Meshack;
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma;
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma;
Mtendaji Mkuu - Wakala wa Mitandao;
Mkurugenzi Mkuu - Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali;
Wakurugenzi wa Wizara na Taasisi za Serikali mliopo;
Wakurugenzi wa Halmashauri mliokuwa hapa;
Wakufunzi na Wataalam wote;
Waandishi wa Habari;
Mabibi na Mabwana.
UTANGULIZI - SHUKRANI NA PONGEZI
Ndugu Washiriki
MANUFAA YA MIFUMO YA PLANREP NA FFARS
Ndugu Washiriki,
WAJIBU, MAELEKEZO NA MAAGIZO
Ndugu Washiriki,
Vilevile, ngazi zote za Mamlaka za Serikali za Mitaa lazima zitoe taarifa za mapato na matumizi kwa Wananchi wanaowahudumia kupitia mikutano, mbao za matangazo, tovuti, vyombo vya habari na njia nyinginezo.
Ndugu Washiriki,
Ndugu Washiriki
Mifumo hii imeshirikisha Wizara za Kisekta na Taasisi za Serikali ikiwemo Wakala wa Serikali Mtandao (e-Government Agency-eGA) kuanzia hatua za awali za ukusanyaji wa mahitaji hadi utengenezaji wa mifumo; hivyo basi, mfumo wa uandaaji wa Mipango na Bajeti(PlanRep) pamoja na mfumo wa Usimamizi wa Fedha katika Vituo vya Kutoa Huduma za Elimu na Afya ndio itakayotumika katika Halmashauri na Vituo vya kutolea Huduma za Jamii. Hivyo, iwapo kuna Mdau anataka kushirikiana na Serikali anapaswa kutumia na kuboresha mifumo hii na siyo kuleta mifumo mingine. Uwingi wa mifumo huondoa ufanisi na uwajibikaji.
Ndugu Washiriki,
Serikali ina matarajio makubwa na mifumo hii, na nitapenda Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Ofisi yangu zipate taarifa zote za Mipango, bajeti pamoja na taarifa za Fedha zinazopelekwa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa wakati na zikiwa katika ubora wa hali ya juu. Aidha, ni vyema sasa mapungufu na dosari zinazojitokeza wakati wa ufungaji wa Hesabu za Mwisho wa mwaka za Halmashauri ziondoke kupitia mifumo hii.
Ndugu Washiriki
Napenda kutumia fursa hii kuwafahamisha Viongozi na Watendaji pamoja na Wananchi wote kwamba, lengo la matumizi ya mifumo ya TEHAMA ni kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi wa shughuli za Serikali na isitumike kukwamisha shughuli au utaratibu wa kazi za Serikali. Hivyo, ni muhimu itumike kwa ufasaha ili kuleta tija inayotarajiwa.
Kwa kuwa mifumo hii ni ya gharama kubwa kila mmoja wenu kwa nafasi yake ahakikishe anailinda, kuitunza na kuitumia mifumo hii ili iweze kudumu na kuwa endelevu kwa manufaa yetu kama Serikali na faida ambazo tutazipata kutokana na matumizi ya mifumo.
Ndugu Washiriki
Pamoja na maelezo niliyotoa pia ninaagiza yafuatayo:-
HALI ILIVYOKUWA KABLA YA MATUMIZI YA MIFUMO
Ndugu Washiriki
Katika taarifa niliyoletewa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI na kwa kuzingatia uzoefu niliopata nikiwa Ofisi ya TAMISEMI, ni kwamba Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kipindi kirefu imekuwa ikitumia gharama kubwa katika kukamilisha zoezi zima la uandaaji wa Mipango na Bajeti. Pia, Halmashauri zimekuwa zikitumia muda mrefu na gharama kubwa kwenye kuandaa na kuwasilisha Bajeti kwenye Mamlaka mbalimbali za Serikali na hata katika ufungaji wa Hesabu.
Hesabu za mwaka 2017/2018 zilizotolewa zinaonyesha kuwa gharama za mchakato wa maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya mwaka kwa Halmashauri 185 ni takriban Shilingi Bilioni 8.32 za kulipia usafiri (Mafuta), posho ya kujikimu, shajala na gharama za kudurufu Vitabu. Gharama hizo hazijumuishi gharama za mawasiliano ya mtandao, Umeme, Simu, matengenezo ya magari na matengenezo ya vifaa vya Ofisi kama vile photocopier, n.k.
Kutokana na gharama hizo, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimepata wakati mgumu kwa kujikuta wakitumia fedha nyingi kugharamia maandalizi ya Bajeti na kusababisha Wananchi kukosa huduma kutokana na Wataalam wa Halmashauri kutumia muda mrefu katika mchakato wa zoezi la bajeti. Aidha, maandalizi ya bajeti yamekuwa na changamoto nyingi na kusababisha Halmashauri kuvuka na bajeti kubwa mwisho wa mwaka, kwa kuwa zoezi huchukua muda mrefu. Changamoto hii itaondolewa na matumizi ya mifumo hii.
MWISHO
Ndugu Washiriki
Ni jambo la kutia moyo kwamba, kupitia mfumo huu wa PlanRep changamoto hizi zimetatuliwa na tutaweza kuokoa wastani wa ShilingiBilioni 4 kila mwaka ambazo ni gharama za Serikali zilizokuwa zinatumika kwa ajili ya kufanya maandalizi na mchakato wa Bajeti kama kuandaa machapisho, nauli pamoja na posho za kujikimu kwa Watumishi wanaoshiriki kuandaa Bajeti za Halmashauri.
Kabla ya kuhitimisha Hotuba yangu, napenda kuwashukuru Wadau Wetu wa Maendeleo wa USAID na Wadau wengine waliochangia Mradi huu na nawaomba tuendelee kushirikiana katika kuimarisha na kuufanya mfumo huu kutumika kwa ufanisi katika Ofisi zote zinazofanya kazi na Halmashauri. Nitumie fursa hii kuwasilisha, kuishawishi Serikali ya Marekani iweze kuingiza Mikoa 13 iliyobaki ili iweze kujumuishwa kwenye Mradi wa PS3. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini mchango wenu na tunaamini kuwa nyie ni wadau wa kweli na kudumu katika kuleta mabadiliko na maendeleo ya haraka katika Nchi ya Tanzania. Tunawashukuru sana.
Baada ya maelezo hayo, sasa nipo tayari kuzindua rasmi Mifumo miwili mipya ya kielektroniki ambayo ni mfumo wa Kupanga Mipango, Kuandaa Bajeti na Kutolea taarifa za hatua za Utekelezaji wa Bajeti (PlanRep - Planning, Budgeting and Reporting System) pamoja na mfumo wa Kufanya Malipo na Kutoa Taarifa za fedha ambazo zimetumwa kwenye Vituo vya Kutoa Huduma (Facility Financial Accounting and Reporting System).
Asanteni Sana kwa Kunisikiliza.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa