Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu, ametembelea na kukagua shughuli za Ujenzi wa zahanati ya Nyakatanga iliyojengwa kwa ufadhili wa Shirika la World Vision, mchango wa Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini, Mhe. Charles Mwajige (MB) na nguvu ya jamii.
Awali kata hii haikuwa na zahanati wala kituo cha afya hivyo ujenzi wa zahanati hii utasaidia wananchi kupunguza kutembea umbali mrefu kwenda kupata huduma za afya.
Mradi huu umegharimu kiasi cha Tsh 56,761,100, kati ya hizo World Vision imechangia Tsh. 47,000,000.00, Mbunge amechangia Tshs. 5,451,000,00 na wananchi wamechangia Tsh. 4,310,000.00.Na uongozi wa Kata unaendelea kuhamasisha wananchi kuchangiz ili kukamilishaujenzi wa kichomea taka na nyumba ya mtumishi.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa