Katika Baraza la Madiwani lililofanyika ndani ya Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Dkt Abel Nyamahanga amelipongeza Baraza hilo kwa kuvuka malengo ya makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2022-2023.
Akizungumza katika Baraza hilo Mkuu wa Wilaya amesema kuwa Halmashauri imefanikiwa kukusanya zaidi kwa asilimia 22.6 ya lengo la mwaka na kufanikiwa kupata hati safi ya ukaguzi wa Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
"Niwaombe na nitoe rai kwenu waheshimiwa Madiwani tuendelee kushikamana ili tuendelee kukusanya zaidi na ili miradi yetu iendelee kutekelezwa kwa wakati na tukipata fedha nyingi tunaweza kupanga miradi mingi na kuitekeleza kadri inavyowezekana" amesema Mhe. Dkt Abel Nyamahanga.
Aidha, ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha miradi yote ambayo haijatekelezwa kwa bajeti ya mwaka 2022-2023 ifanyiwe utekelezaji kwa wakati na taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo ipelekwe Ofisini kwake ili waweze kufatilia kuona namna miradi hiyo ilivyotekelezwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mhe. Magongo Justus ameleeza kuwa asilimia 40 ya makusanyo ya mapato ya ndani imerudishwa kwenye utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo.
Sambamba na hayo ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama kwa namna wanavyosimamia na kuhakikisha wanahamasisha amani ndani ya Wilaya ya Muleba.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa