Halmashauri ya Wilaya ya Muleba leo tar 3 Julai, 2024 imepokea tuzo ya ulipaji na ununuzi wa dawa na Vifaa Tiba kwenye vituo vyake vya afya kwakutumia mapato ya ndani.
Tuzo hiyo imetolewa na Meneja wa Bohari ya Dawa na vifaa tiba (MSD) Kanda ya Kagera ndugu Kalendero Masatu na kupokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba ndugu Isaya Mbenje ofisini kwake.
Tuzo hiyo ya pongezi na shukrani imetolewa kama ishara ya kuthamini mchango wa Halmashauri ya Muleba kwenye ununuzi wa dawa na Vifaa tiba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu: 0744644702
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa