Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Ndg. Elias Kayandabila amefanya ziara ya kutembelea na kukagua mwitikio wa wazazi kuwapeleka shule za awali katika shule ya mpya shikizi Daraja nane na shule mpya shikizi Kashenye.
Akizungumza na wazazi waliwaleta wanafunzi kuanza masomo ya awali katika shule ya msingi shikizi Daraja nane amewasihi na kuwasistiza wazazi ambao hawajawapeleka watoto shule wakawapeleke watoto wao shule.
"Wale ambao hawajawaleta watoto wambieni sasa wazazi wawalete watoto" amesema Mkurungenzi Mtendaji Ndg. Elias Kayandabila.
Lakini pia ameongeza kwa kuwambia kuwa wametenga kiasi cha milioni sita na laki tatu kwa ajili ya ujenzi wa vyoo ambapo amewaomba wasaidie kuchimba hivyo vyoi ili hiyo pesa isaidie kujengea vyoo hivyo.
Kwa upande wao wazazi katika nyakati tofauti tofauti wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule shikizi jambo ambalo limewasaida wazaz hao watoto wao kusomea katika madarasa bora pamoja na kusistiza kuwa wataendelea kuwasisitiza wazazi ambao hawajawapeleka watoto wao shule kuendelea kuwapeleka watoto shule.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa