Katika Baraza la madiwani lililofanyika ndani ya,Ukumbi wa Halmashauri Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Elias Kayandabila pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Magongo Justus wamekabidhi Kompyuta 42 kwa Maafisa elimu Kata wa wilaya ya Muleba zilizotolewa na Serikali kwa lengo la kuboreha Elimu.
Akizungumza baada ya kukabidhi Kompyuta hizo Mkurugenzi Mtendaji ametoa wito kwa Maafisa Elimu waliokabidhiwa Kompyuta kuzitumia kompyuta kwa matumizi ya Ofisi na kuwa hawatarajii kuona Komyuta zimeenda kutumika kwa ajili ya matumizi binafsi.
"Niwaombe Komyuta hizi mkazitunze kwa sababu hivi ni vifaa vya Kierektroniki hivyo havihitaji unyevu na maji kwa maana hiyo mkazitunze vizuri ili ziweze kukaa kwa mda mrefu ili ziweze kutunufaisha na kuwanufaisha Watanzania kwa ujumla kwahiyo nawaomba muendelee kuwa makini zaidi katika utunzaji wa Kompyuta hizi" amesema Ndg. Elias Kayandabila.
Lakini pia Mkurugenzi Mtendaji ameeleza kuwa lengo kubwa la Serikali ni kuboresha taarifa kwa maana ya kuwa na takwimu sahihi za ufundishaji na miundombinu yote ambayo inahitajika kwa ajili ya elimu hivyo Kompyuta hizo zimetolewa kwa matumizi ya ofisi ili ziweze kufanya kazi na kurahisisha mawasiliano.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Mhe. Magongo Justus ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais. Samia Suluhu Hassan kwa kuelewa na kuona uhitaji wa Halmashauri kwa kutoa Kompyuta kwa Maafisa Elimu Kata.
"Hili lililofanywa na Serikali litatusaidia sana kupunguza matumizi ya Karatasi, kuandika kwa mkono na pia zitaweza kusaidia katika utunzaji wa takwimu mbalimbali kwa shule zetu za msingi na Sekondari hivyo niwaombe Maafisa Elimu kuzitunza Kompyuta hizi" amesema Mhe. Magongo Justus
Khalib Issa Mtabazi Afisa Elimu kata Nyakatanga ameeleza kuwa kupitia msaada huo yeye binafsi amefarijika kwa sababu itaweza kumsaidia katika ukusanyaji wa takwimu na pia kuisaidia wilaya ya Muleba kukusanya takwimu ambazo ni sahihi.
Naye Mwl. Meriness Kaizilege Maruka Afisa elimu Kata ya Mayondwe ameipongeza serikali kwa kurifikilia na kuona umuhimu kwamba sasa wanastahili kupatiwa vifaa vya kompyuta hivyo itaweza kuwasaidia Sana katika masuala ya mtandao na taarifa nyingine mbalimbali ambazo inabidi zifanyike kimtandao.
Sambamba na hayo ameeeleza kuwa changamoto waliyokuwa nayo awali walipokuwa wanapata changamoto ya kompyuta ilikuwa inatakiwa kuomba msaada kwa wenye kompyuta na wakati mwingine iliwalazimu kwenda kwenye Steshenari ili kupata huduma za kimtandao.
Serikali imetoa Kompyuta 42 aina ya (LENOVO) kwa wilaya ya Muleba kwa Maafisa elimu Kata ambapo kila Kompyuta moja inagharimu kiasi cha shilingi Milioni mbili na laki tano 2,500,000/= hivyo Kompyuta zote zinazokadiliwa kugharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100/=
Imeandaliwa na kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa