Mkuu wa Wilaya ya Muleba kwa sasa Mh. Toba Alnason Nguvila ambaye amekaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya Muleba kwakufikia kiwango cha kuwa miongoni mwa Halmashauri zenye hati inayoridhisha.
Mh. Nguvila amezungumza hayo kwa mara ya kwanza wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha kujadili hesabu za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera.
Mh. Nguvila ameeleza kuwa alipokea taarifa ya Mkaguzi wa hesabu za serikali(CAG) ya mwaka 2019/20 na kubaini kuwa Halmashauri ya wilaya ya Muleba ni moja kati ya Halmashauri sitaza mkoa wetu zilizopata hati inayoridhisha.
"Nilipokea taarifa ya (CAG) ya mwaka 2019/20 na baada ya kusoma nimebaini kuwa Halmashauri ya wilaya ya Muleba ni moja kati ya Halmashauri sita za Mkoa wetu zilizopata hati inayoridhisha".Amesema Mh. Nguvila.
Ameongeza kwa kueleza kuwa Mkaguzi alibainisha masuala mawili ya msisitizo katika taarifa yake kwa Halmashauri ya Wilaya Muleba ambayo watendaji waliyafanyia kazi na kuwasilisha kwa mkaguzi."Matokeo haya ni matunda ya ushirikiano baina ya viongozi na watendaji, ofisi ya Mkuu wa Wilaya na vyombo vyote vya usalama katika kusimamia raslimali za umma na uwajibikaji katika wilaya yetu ya Muleba" Ameongeza Mh. Nguvila.
Lakini pia Mh. Nguvila amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba, wakuu wa Idara na vitengo vyote pamoja na waheshimiwa madiwani wote wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba kwa uongozi na utendaji mzuri na kuwatakia kuendeleza umoja na Mshikamano kwa manufaa ya wananchi wa Muleba.
Kwa upande mwingine Mh. Nguvila amesema kuwa kwa Halmashauri inayofanya vizuri ni halmashauri ya wilaya ya Muleba na kuitaka Halmashauri kulinda hali hiyo ili kuweza kuendelea kuwa vinara kila mwaka na amehaidi kuwa yote haya yatatokana na mshikamano, ushirikiano, upendo, utulivu na kusimamia vizuri wataalamu.
Aidha, Mh. Nguvila amewaomba madiwani kuendelea kushirikiana na ofisi ya mkuu wa Wilaya katika kutatua changamoto zinazojitokeza hususani za kimaendeleo na hata za kitaalamu ili kuongeza udhibiti wa mapato yanayokusanywa pamoja na kuimarisha usimamizi wa raslimali utumishi na fedha za miradi ili kupata thamani ya fedha na wananchi kupata manufaa ya miradi husika kwa wakati.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa