Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila amewaagiza Kikosi cha Askari wa polisi pamoja na viongozi wa NARCO. wanaohusika na oparesheni ya kuwaondoa wakazi wasiolasmi kwenye maeneo ya vitalu vya Mifugo kufuata utaratibu ili amani iweze kuendelea kuwepo katika kata ya Rutolo iliyopo katika eneo la lanchi ya Mifugo ya Kagoma.
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa wilaya Baada ya kwenda na kufika sehemu hiyo na kukuta wakazi wa eneo hilo wakilalamika kuchomewa na nyumba zao na mashamba yao kufyekwa na askari wanaohusika na oparesheni hiyo.
"Sihitaji machafuko kwenye wilaya ya Muleba sihitaji mauaji kwenye wilaya ya Muleba hatuwezi kila siku tukawa tunashinda Rutolo ni lazima ifike hatua tuweke utaratibu mzuri ili kusudi amani iwepo" amesema Mhe" Toba Nguvila.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ameongeza kwa kusema kuwa vijiji vile vya Rutolo, Kyobuheke, Byengeregere na kijiji cha Zambia ni vijiji ambavyo vinafahamika ambapo amesema kuwa katika vijiji hivyo kama kuna Senta senta ambazo zina watu wabaki labda tu kwa maeneo ambayo watu watakuwa wamejenga nyumba moja moja maeneo hayo watu wasibaki.
Lakini pia Mhe Mkuu wa wilaya amewahimiza watu wa NARCO kuhakikisha wanajiridhisha na usalama wa eneo kwa kuhakikisha wanaangalia usalama wa eneo pamoja na kutambua wanaoingia wageni na wanaopangisha ni wat u wa aina gani ili kuweza kuepukana na mapungufu yanayoonekana sasa hivi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Muleba Ndg. Athuman Kahara amewaomba Shirika la NARCO pamoja na wawekezaji kuwa wazalendo kuhakikisha na wao wanashiriki kwa namna mbalimbali katika kuchangia maendeleo ya wananchi na wilaya kwa ujumla.
Naye Afisa TAKUKURU wa wilaya ya Muleba Ndg. Said Lipunjaje ameomba oparesheni iendelee kwa kuzingatia maelekezo waliyopewa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanarinda haki za mwanadamu na kwa yale mapungufu ambayo yapo yafanyiwe.
Mwisho Kiongozi wa kikosi kinachohusika na oparesheni hiyo amesema kuwa watafanya kazi vizuri hasa kwa kuzingatia kile ambacho wameelekezwa kutekeleza ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanarinda masilai ya nchi, masilai ya Watanzania pamoja na masilai ya wawekezaji.
Imeandaliwa na kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa