Katika zoezi la uteketezaji wa Nyavu haramu lilifanyika katika Kata ya Nyakabango Kijiji Katembe Mwalo wa Magarini Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Mhe. Dr Abel Nyamahanga ametoa onyo kwa viongozi wanaoshiriki katika vitendo vya uvuvi haramu kuacha tabia hiyo.
Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo Mkuu wa Wilaya amesema kuwa kama kiongozi yeyote atabainika akijihusisha na uvuvi haramu hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
"Yeyote ambaye ni kiongozi na anataka kulinda heshima yake ya uongozi afuate maadili ya uongozi ukishakuwa kiongozi lazima uuambie moyo wako utulie ufanye kazi za uongozi na uwe na maadili ya uongozi na sio vinginevyo kushiriki kwenye uvuvi haramu kama serikali hatuwezi kunyamaza kimya tutachukua hatua za kisheria" amesema Mhe. Dr Abel Nyamahanga.
Aidha, Katika oparesheni hiyo amemsimamisha kazi ya Uenyekiti aliyekuwa Mwenyekiti wa BMU Katika Mwalo huo Ndg. Thobias Masebwe pamoja na mjumbe wake Ndg. Juma Salumu kwa tuhuma za kufanya wizi wa kamba za mitego haramu na kuzirudisha eneo la kuchomea nyavu haramu baada ya kuwa wamebainika.
Kwa upande wake Ndg. Stanslaus Joseph Mwenyekiti wa Kitongoji Kasheza amesema kuwa nyavu haramu zinaharibu na kuua mpaka samaki wachanga kabisa ambao hawafai hata kuvuliwa hivyo ameiomba Serikali kuwezesha upatikanaji wa nyenzo zitakazotumika kupambana na uvuvi haramu.
Naye Charles Isaka Mkazi wa Magarini amesema kuwa kutokana na kushamili kwa vitendo vya uvuvi haramu vimepelekea upatikanaji wa samaki kuwa adimu tofauti na ilivyokuwa awali jambo ambalo limesababisha hata samaki kupanda bei tofauti na ilivyokuwa awali.
Katika taarifa iliyosomwa na Afisa Uvuvi wa Wilaya ya Muleba Ndg. Wirifred Tibendelana ameeleza kuwa katika doria 28 zilizofanyika kwa kipindi cha miezi mitatu jumla ya kokoro 80, nyavu za timba 217, nyavu ndogo za makila 320, tupatupa 3 zimekamatwa katika doria hiyo na nyavu hizo zote zinakadiliwa kuwa na thamani ya jumla ya kiasi cha Tsh. milioni 97.7.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mahusiano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa