Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe Dkt. Abel Nyamahanga amemaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa mda mrefu kati ya kijiji Bureza kilichopo Kata ya Bureza na Kijiji Kasheno Kilichopo kata ya Magata Karutanga.
Mkuu wa Wilaya amewaeleza wananchi kuwa Mgogoro huo ulikwisha tatuliwa na uongozi wa wilaya kwa kikao kilichofanyika tarehe 28/05/2019 na kuhudhuliwa na viongozi wa vijiji hivyo pamoja na waheshimiwa madiwani na kwa mujibu wa barua ya tarehe 04/06/2010 Halmashauri za vijiji vyote viwili vilipewa maelekezo kuwa mipaka wa vijiji hivyo inatengwa na mabonde.
Aidha, ameusihi uongozi wa Halmashauri ya Kijiji Bureza na Kijiji Kasheno kuheshimu utatuzi wa mgogoro huo kama ulivyotatuliwa mwaka 2010 na kuisihi Halmashauri ya Kijiji Bureza kuendelea kuitunza mipaka na kuzuia uvamizi wa ardhi na kuendelea kuitumia ardhi hiyo kama ilivyoanishwa kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi ya Kijiji cha Bureza.
''Naomba wananchi wote tuheshimu maamuzi ya utatuzi wa mgogoro huu na sitegemei kama ntarudi hapa watendaji wa vijiji, watendaji wa Kata wenyeviti wa Vijiji naombeni myasimamie haya sitegemei kurudi hapa nikirudi ntarudi kwa namna nyingine" amesema Mhe Dkt. Abel Nyamahanga.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Magata Mhe. Yakubu Mahamudu amesema wataendelea kuheshimu na kufuata taratibu pasipo kuleta migogoro kama alivyoagiza Mkuu wa Wilaya.
Naye Diwani wa Kata ya Bureza Mhe. Diocres Nsinde amewasihi wananchi wa vijiji hivyo kuendelea kuwa na ushirikiano wa pamoja na kuendelea kutunza mipaka hiyo kama ilivyoelekezwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa