Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Dkt Abel Nyamahanga amewasihi wajumbe waliohudhulia katika kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi kwenda kutoa elimu kwa wazazi wa watoto wenye umri chini ya miaka 8 kuhakikisha wanajitokeza ili watoto wao waweze kupata huduma ya chanjo ya polio.
Akizunguza katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya amesema kuwa elimu ikitolewa kwa wazazi na walezi wa watoto wataona umuhimu wa watoto wao kuchanja chanjo ya Polio ambayo itawalinda dhidi ya maambukizi ya virusi vya Polio.
"Tusisite kuwambia tuwambie wananchi juu ya umuhimu na madhara ya kutochanja watoto chanjo ya polio" amesema Mhe. Dkt Abel Nyamahanga.
Katika Tarifa iliyosomwa na Mratibu wa Chanjo ya Polio Wilaya ya Muleba Bi. Christina Mlemi ameeleza kuwa ugonjwa wa pllio umelipotiwa katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa mnamo tarehe 29/06/2023 kwa mtoto wa umri wa muaka mmoja na miezi 11 ambaye vipimo vyake vilipelekwa maabara ma kutoa majibu chanya.
Hivyo, kutokana na mlipuko huo Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa tokomeza Polio waliamua kampeni hii ifanyike katika Mikoa sita ambayo inamuingiliano ambayo ni Kagera,Katavi,Kigoma, Rukwa, Mbeya, na Songwe.
Aidha, ameongeza kwa kusema kuwa ugonjwa wa Polio husababishwa na virusi vya polio ambavyo husababisha mtoto kulemaa na huingia mdomoni kwa njia ya kunywa maji au kwa njia ya kula vyakula ambavyo vimechafuliwa na kinyesi, mtoto asiyepata chanjo ya polio ni hatari katika maisha yake yote na jamii nzima kwa ujumla kwa sababu huambukizwa kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mtoto mwingine.
Akizungumzia lengo la Kampeni ya Polio ni kuongeza uelewa kwa wanajamii kuhusu faida za chanjo ya Polio ambapo chanjo ya polio ndio kinga pekee ambayo inaweza kumlinda mtoto dhidi ya ugonjwa huo.
Kampeni hii itaanza rasmi kuanzia tarehe 21-24/09/2023 kwa ajili ya kuwalinda na kuwazuia watoto wote chini ya miaka 8 kuenea kwa virusi vya Polio na kupitia Kampeni hii Halmashauri ya wilaya ya Muleba inalenga kuwachanja jumla ya watoto laki 160,324.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa