Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila amesisitiza na kuhimiza watumishi wasaidizi wa ofisi kupewa kipaumbele na kuwajali katika masuala mbalimbali katika kikao kilichofanyika ndani ya Ukumbi wa Halmashauri baina ya Mkuu wa wilaya na watumishi wa serikali ili kutatua kero zao.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa wilaya amewaomba wakuu wa Idara kukaa vizuri na watumishi wasaidizi kwani hata wao wanasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kazi za kiofisi.
"Ni vizuri mkawa na desturi ya kuwajali hawa watumishi wasaidizi wa ofisi kwa sababu ni watu muhimu msipowajali mtaumia wenyewe siku moja, sitaki nisikie malalamiko kutoka kwa hawa kwahiyo ni vizuri mkawazingatia" amesema Mhe. Toba Nguvila.
Aidha, Mkuu wa wilaya amuagiza mdhibiti mkuu wa ubora wa shule wilaya ya Muleba kuwa anatembelea na kukagua maendeleo ya shule ili kufuatilia maendeleo ya taaaluma katika shule zote za wilaya.
Sambamba na hayo amewaagiza Maafisa Tarafa, Waratibu elimu wa Kata na Watendaji wa Kata kuhakikisha wanawahimiza wazazi kuchangia vyakula mashuleni ili kuwawezesha wanafunzi kufaulu vizuri kupitia uwepo wa huduma ya chakula cha mchana wawapo mashuleni kwani itawasaidia kusoma na kuelewa wanayofundishwa na walimu wawapo mashuleni.
Lakini pia amewaagiza walimu wa michezo kusimamia vizuri michezo mashuleni ikiwa ni pamoja na michezo ya UMISETA na UMITASHUMITA ili kuweza kuwapata vijana ambao wana uwezo mzuri katika michezo mbalimbali.
Mkuu wa wilaya amesema kuwa ni lazima iwepo mikataba kwa walimu ya kuongeza ufauru kwa wanafunzi ili waweze kuongeza jitihada katika kufaurisha wanafunzi ili Wilaya ya Muleba iweze kufanya vizuri na kuwa ya kwanza kitaaluma jambo ambalo amesema linawezekana kama hatua hiyo itachukuliwa.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Ndg. Charles Ntaki amesema kuwa suara la chakula mashuleni kwa wanafunzi ni suara muhimu sana hivyo ni muhimu wazazi kuchangia chakula mashuleni, lakini pia amesema ofisi ya Mkurugenzi walishagiza uanzishwaji wa mashamba mashuleni ya kuzalisha nafaka ili suara la kuwagalamia watoto chakula liweze kuwa jepesi.
Naye Afisa Utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Ndg. Christopher Donatus amewaomba watumishi wote kutambua kwamba wao ndio wasadizi wakubwa wa Mkurugenzi na Mkuu wa wilaya katika kusimamia rasilimali zilizopo katika wilaya ya Muleba pamoja na kusimamia watumishi hivyo ni wajibu wao kuwa na nidhamu na maadili ya kiutumishi ikiwa ni pamoja na kuwasimamia hata watumishi wengine waliopo katika ngazi za chini.
Mdhibiti ubora wa shule wilaya ya Muleba Ndg. Josephat Masiko ameomba viongozi wa ngazi ya shule wasimamie kuandaa mpango wa jumla wa maendeleo ya shule ambao unatekelezwa kila baada ya miaka mitatu unawaoshirikisha viongozi wote wa kijiji ili kuweza kupunguza matatizo ya shule.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa