Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila katika ziara yake alipovitembelea vijiji vya kata ya Rutolo wilayani Muleba amewahimiza viongozi wa Tarafa, Kata, Vijiji na Vitongoji wa Rutolo kuhakikisha wanasimamia ili kuzuia watu kuingia kinyume na utaratibu katika eneo hilo.
Akizungumza katiza ziara hiyo alipovitembelea vijiji vinne vya kata ya Rutolo ambavyo ni Byengeregere, Rutolo, Kyobuheke na Nshabya amewasihi wananchi kuhakikisha hawaruhusu watu kuingia kinyume na utaratibu katika eneo hilo bila idhini yake Mkuu wa wilaya ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kuruhusu mtu aingie au asiingie ambapo amewaeleza kuwa mwenye idhini ya kuingiza watu na hata Mifugo ni yeye Mkuu wa wilaya na Kamati yake ya usalama.
"Niwaagize viongozi wote wa tarafa wa kata wa vijiji wa vitongoji kwenye hili msimamie mseme sasa basi hajuhitaji kuingiza ingiza watu kinyemela ninyi mliopo mnatosha kama watu wanaingia wafuate utaratibu" ameendelea kusema.
"Ni lazima ifike hatua mkae vizuri mfanye shughuli zenu za kiunchumi, kijamii, na za kisiasa bila kuwa na mitafaruko mitafaruko haijengi utengamao kwenye eneo na ndio maana tuko hapa tumeamua tumedhamilia sasa hizi hofu hofu mda wote ziishe sasa" amesema Mhe Toba Nguvila.
Aidha, amewaeleza wananchi wa Rutolo kuwa wameshaka na NARCO pamoja na kamati ya usalama na waziri wa mifugo na uvuvi ambapo walikubaliana namna ya kuwapanga katika maeneo mazuri ambayo wanaweza wakalima na kuzalisha ili kuepuka njaa ambapo amewaeleza kuwa itakuja kamati ambayo itakuwa na wataalamu wote wa kubainisha maeneo bora ya wao kulima.
"Kwa wale ambao tutawatoa kutoka maeneo ya mbali ambao wataathirika kuletwa kwenye haya maeneo watatengewa hekali sita sita kila familia ili wajenge na wapate sehemu ya kulima jambo la msingi viongozi wote wa kata wa vijiji wa vitongoji mshiriki kikamilifu kwenye zoezi ili msaidie kurahisisha kazi ya kamati kamati itakuja hapa ninyi muikumbatie muwe marafiki ili zoezi liwe rahisi liishe haraka" amesema Mhe. Toba Nguvila.
Lakini pia amewaomba na kuwasisitiza wananchi wa eneo hilo kuhakikisha wanakuwa walinzi wakubwa wa vitalu kwa sababu vitalu vinaenda kupunguzwa kwa ajili yao ambapo amewambia kuwa wakishapangwa vizuri wawe marafiki na wenye vitalu ambao watawasaidia ili hata wakati wanajenga shule wawasaidie kuchangia saruji na mabati.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Muleba Kaskazini Mhe. Charles Mwijage amewaeleza kuwa wakiwa karibu kutoka maeneo ya mbali huduma za kijamii zitaweza kuwafikia kila mwananchi ikiwa ni pamoja na umeme na maji ambapo amewaeleza kuwa wakikaka kwa kutawanyika itakuwa ni vigumu hata kuwepo kwa urahisi kwa walioko mbali kupata huduma za umeme, maji pamoja na shule.
Mwisho, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Muleba Mhe. Athuman Kahara amewaeleza wananchi wa eneo hilo kuwa kwa walio mbali wanakwenda kupangiwa maeneo mazuri ya kilimo ambayo yatawasaidia kulima na kuzalisha miaka yote pamoja na vizazi vyao vyote.
"Unapoona unakwenda kumiliki kile ambacho ni halali hiyo ndo faida mtakayoipata tangu leo sisi kama chama pamoja na serikali wale wote watakaotengewa maeneo ya hekali sita sita ni wale ambao watakuwa kwenye maeneo tayari adui watakuwa ni wale watakaukuja kupangiwa wakakutwa walikuwa hawana makazi kabla ya kugawiwa maeneo" amesema Mhe. Athuman Kahara.
Imeandaliwa na kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa