Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Rulanda Kata ya Rulanda wilayani Muleba amehimiza wanawake kupewa fursa mbalimbali za kimaendeleo ili kuondoa ongezeko la wimbi kubwa la wanawake wanaoishi katika hali ya umaskini.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa wilaya ya Muleba amesema kuwa wanawake wakipewa fursa mbalimbali itawasaidia kupata ajira, kuongezeka kwa vipato katika familia na kuondoa wimbi kubwa la jamii inayoishi katika umaskini.
"Ni lazima sisi kama Serikali tuone namna ya kuwasaidia wanawake na ni jukumu letu kuhakikisha wanawake wote bila kujali hali zao wanapata haki zao zote za msingi zinazohitajika kwa ajili ya kuleta maendeleo chanya katika uchumi wa viwanda"
Aidha, Amewaomba na kuwahamasisha wanawake wa wilaya ya Muleba kuanzisha vikundi na kukopa fedha kutoka Halmashauri kwa ajili ya kuanzisha biashara na miradi mbalimbali itakayosaidia kuinua hali zao kiuchumi.
Lakini pia amewaomba wananchi kujitokeza katika zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika kitaifa mwezi wa nane mwaka huu ili serikali iweze kujua idadi ya watu wote katika nchi kwa umri wao jinsia mahali wanapoishi na hali ya elimu hali ya ajila na hali ya vizazi na vifo pamoja na hali ya makazi ili kupitia takwimu hizo serikali iweze kuainisha mahitaji ya msingi ya wannchi na taifa kwa ujumla.
Sambamba na hayo amewaeleza wanawake kuwa ni watu muhimu kwenye familia na jamii kwa ujumla hivyo wanatakiwa kusimama kwenye nafasi yao kuisaidia jamii na Tanzania kwa ujumla kwasababu wao ndio nguzo ya kweli walezi na ni kioo kwenye jamii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Mhe. Magongo Justus amewaomba wanawake wote kupitia siku hiyo ya wanawake iwahamasishe kuwa walimu wa kweli walinzi wa kweli na wawe pia wazazi wa kweli pamoja na kuifanya dunia iwe nimahara salama na bora pa kuishi.
Katika risala yao iliyosomwa na Bi. Asuma Abdalah wameomba kuwawezesha wanawake kufikia Tanzania ya viwanda ni lazima kuwe na uwekezaji katika sekta ya kilimo hivyo wameomba kusaidiwa kupata pembejeo huduma za ugani kutafta masoko na juhudi hizo ziende sambamba na upatikanaji wa teknolojia rahisi ya uzalishaji mali katika kukamilisha mzunguko wa myororo wa thamani ili kuchangia ipasavyo katika Tanzania ya viwanda.
Lakini pia wameomba kutengewa eneo ambalo lutakuwa eneo la uzalishaji hasa katika nyanja ya viwanda pamoja na kuwa na miundombinu ya umeme maji barabara na kadhalika
Kauli Mbiu ya Mwaka huu inasema kuwa "Kizazi cha haki na usawakwa maendeleo endelevu tujitokeze kuhesabiwa" kauli mbiu inasisitiza umuhimu wa usawa wa kijinsia katika kuleta maendeleo ya kweli na yanayonufaisha makundi yote katika jamii hapa nchini pamoja na kuwakumbusha wananchi kushiriki katika zoezi la sensa ya idadi ya watu na makazi.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa