Katika Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani iliyofanyika Kata ya Kamachumu Kijiji cha Bulamula Wilaya ya Muleba Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Dr Abel Nyamahanga amewahimiza wananchi kulinda na kutunza miundombinu ya maji ili iweze kudumu kwa mda mrefu.
Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi katika tenki la Mradi wa Maji wa Bulamula amewaeleza wananchi kuwa ni wajibu wao kulinda miundombinu ya maji dhidi ya uhalifu ambao unaweza kujitokeza.
"Wapo watu wengine sehemu linakopita bomba la maji wanajenga nyumba huu sio utaratibu na wala sio usitaarabu tusifanye hivyo pahala penye bomba la maji tujenge pembeni hivyo niwasihi muepuke kujenga na kulima kwenye miundombinu ya maji ili miundombinu hii iendelee kutuhudumia kwa mda mrefu " amesema Mhe. Dr Abel Nyamahanga
Aidha, Mkuu wa Wilaya amewahimiza wananchi wa Kijiji cha Bulamula kuwa kukamilika kwa mradi huo kulete tija katika kuchangia mabadiliko chanya ya uchumi endelevu ambapo amewasihi kuwa maji yatumike na yalete thamani katika kukuza shughuli za kiuchumi.
Lakini pia amewahimiza wananchi kupanda miti katika vyanzo vya maji ili kusaidia kutunza maji na kuchangia upatikanaji wa maji katika vyanzo hivyo.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa RUWASA Mkoa wa Kagera Mhandisi Patrice Jerome ameeleza kuwa kwa kipindi cha Miaka Miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan hali ya huduma za maji imeendelea kuimalika wilayani Muleba ambapo zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa Wilaya ya Muleba wanapata huduma za maji.
Pamoja na hayo ameongeza kwa kusema kuwa zaidi ya miradi 11 inatekelezwa katika Wilaya ya Muleba ambapo kati ya miradi hiyo kuna miradi imekamilika na imeshaanza kutoa huduma na kuna miradi inaendelea kutekerezwa na jumla ya vijiji 27 vinaenda kunufaika na miradi hiyo ya maji inayotekelezwa kwa gharama za kiasi cha Tsh. Bilion 11 na zaidi ya wanachi elfu 75178 watanufaika na miradi hiyo.
Katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ametembelea na kukagua chanzo cha Mradi wa Maji wa Ilemera unaotekelezwa kwa kiasi cha Tsh. Milioni 599, tenki la Mradi wa Maji Kagoma unaotekelezwa kwa kiasi cha Tsh. Milioni 680 pamoja na kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa Maji Bulamula unaotekelezwa kwa kiasi cha Tsh. Milioni 681.
Imetolewa na:
Kitengp cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa