Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila amezindua rasmi shughuli za utoaji wa huduma za afya unaofanywa na Meli ya Jubilee Hope inayomilikiwa na Kanisa la African Inland Church Tanzania katika kisiwa cha Chakazimbwe Kata ya Ikuza wilayani Muleba.
Akizungumza baada ya uzinduzi wa Meli hiyo Mkuu wa wilaya ya Muleba amewaomba wananchi wa kisiwa cha Chakazimbwe kuendelea Ku to a ushirikiano mkubwa kwa kanisa la African Inland Church Tanzania na kuwasihi kuwatangazia wenzao kuja kupata huduma za afya katika meli hiyo ili waweze kupona maradhi mbalimbali.
"Ndugu zangu changamkeni kupata tiba katika Meli hii Mungu amewapendelea ninyi ukiwa unaumwa, unakohoa, unajisikia tumbo kuuma au ukajisikia homa nenda kapime uwe na bima uwe huna bima unakwenda unapata huduma bure bila malipo" amesema Mhe Toba Nguvila.
Aidha, Mhe Mkuu wa wilaya amewaomba Madiwani, Watendaji na Wenyekiti wa vijiji na Vitongoji wa kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kuilinda huduma hiyo lakini pia amewaagiza wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama kuweka vyombo vinavyoonekana na visivyoonekana kuhakikisha kuhakikisha kwamba hakuna hujuma yeyote wala mtu yeyote wa kuhujumu huduma ya afya inayotolewa na Meli ya Jubilee Hope pamoja na kuhakikisha wanaweka ulinzi kwa wataalamu wanaotoa huduma katika Meli Hiyo.
"Msipoilinda hii Meli ninyi maana yake mnajinyima wenyewe kupata huduma bora ya afya kupitia Meli hii na wataalamu wake kwahiyo ulinzi wa hawa uwe kwenu" amewasihi wananchi Mhe. Toba Nguvila.
Lakini pia Mhe. Mkuu wa wilaya amewaomba watoa huduma katika Meli hiyo kuendelea kutoa huduma nzuri na bora chini ya usimamizi wa Kanisa la African Inland Church kwa ushirikiano wa Serikali ya wilaya ya Muleba na kuwahaidi kuwa kama serikali watahakikisha kuwa watakuwa salama mda wote ili waendelee kutoa huduma bora kwa wananchi wa Muleba.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Ndg. Elias Kayandabila amewaeleza wananchi kuwa kwa sasa zipo jitihada ambazo zinafanywa na wilaya kuhakikisha wanasuruhisha tatizo la huduma kwenye sekta za afya ambapo amewaeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2022- 2023 tayari Halmashauri imeanza ujenzi wa kituo cha afya kwenye kata ya Bumbile kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri.
Mkurugenzi Mtendaji pia amewaeleza kuwa tayari zimeshapelekwa pale Milioni 350 ili kujenga kituo cha afya na kuwaeleza kuwa Kabla ya mwaka kuisha zitapelekwa milioni 150 kwa ajili ya kituo hicho cha afya.
Sambamba na hayo Mkurugenzi Mtendaji ametoa shukrani kwa kanisa la African Inland Church pamoja na taasisi ya Vine Trust iliyopo Wingereza pamoja na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (Geita Gold Mining GGM) na Serikali hasa Mhe Rais kwa kuweza kukubali kuletwa kwa chombo cha Meli ya Jubilee kuwahudumia wananchi wa Muleba.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Mhe. Justus Magongo ametoa Shukrani kwa Meli kanisa la African Inland Church kwa huduma ya afya wanayoitoa kwa watu wa visiwani lakini pia kwa niaba ya wananchi wa Muleba Amemthibitishia makamu baba askofu wa kanisa hilo Mchungaji Obed Nkulukulu kwamba Muleba wako Tayari kuendelea kushirikiana kwa namna yeyote na shughuli inayoendelea katika Meli ya Mv Jubilee Hope kwa kuwaeleza kuwa kama kutakuwa na hitaji la msaada wowote Kutoka Halmashauri ya Muleba kuwa wako tayari kutekeleza.
Naye Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Theonest Thadeo amewapongeza sana watumishi wa Meli ya Mv Jubilee kwa kujitoa kwa dhati kutumikia eneo la visiwani pamoja na kutoa shukrani za kipekee kwa Mgodi wa Geita (GGM) na Shirika Vine Trust kwa kuchukua jukumu la kutoa huduma za afya kwa kuliona na Kutoa kipaumbele kwa ajili ya afya za wananchi wa Visiwani.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa