Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila amepiga marufuku na kuagiza TAXI bubu zilizopo Muleba zote ziondolewe ili kupunguza changamoto kwa madereva wenye vyombo vilivyosajiliwa kukosa abilia kutokana na uwepo wa TAXI bubu alipokutana na Madereva katika Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba.
Akizungumza katika Mkutano huo amemuagiza OCD kushirikiana na Afisa Biashara kuhakikisha TAXI zinakuwa na maegesho yake na kwenye maegesho hayo ameagiza zipaki TAXI ambazo zimesajiliwa sio TAXI bubu.
" TAXI bubu ambazo hazilipi kodi ya Serikali na hata mfumo wa LATRA hazifahamiki iko hatari wanaweza kupakia abiria wakapotea naye kwa sababu hawatambuliki popote kwahiyo kuanzia leo sitaki kuona TAXI bubu ndani ya wilaya yangu ya Muleba." amesema Mhe. Toba Nguvila.
Aidha Mkuu wa wilaya amemuagiza OCD kuhakikisha stendi anawekwa polisi kwa ajili ya kulinda amani na kusimamia watu na mali zao mda wote magari yatakapokuwa yanaingia na kushusha mizigo pale kwenye stendi kuu ya Muleba.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Muleba Ndg. Greyson Mwengu amewaomba Madereva kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa pale watakapokuwa wanachangamoto ili vyombo viweze kuchukua hatua za kisheria ili kuweza kuondoa changamoto ya TAXI bubu
Naye Shedrack Malale Afisa mfawidhi wa Latra Mkoa wa Kagera ametoa ufafanuzi kwa kuwaeleza Madereva kuwa Sheria ya TAXI inamtaka mwenye TAXI kuchora mkanda kwenye TAXI yake kuweka TAXI (kebo) kiashiria cha TAXI pamoja na kuwa na namba ya Ubavuni inayotolewa na Halmashauri.
Afisa Biashara wa wilaya ya Muleba amewaeleza Madereva kuwa egesho linalotumika kuegesha magari aina ya TAXI ni egesho ambalo lipo kisheria na kuongeza kuwa changamoto iliyopo ni kuhakikisha TAXI zote ambazo hazina usajiri kuondolewa.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa