Mkuu wa chuo cha VETA Ndolage Eng. Machumu K. Machumu ameomba ushirikiano na uongozi wa Halmashauri
ya Wilaya Muleba kukipa hadhi chuo cha VETA Ndolage kuwa Chuo cha wilaya katika siku ya madhimisho ya wiki
ya Utumishi wa Umma alipotembelewa Chuoni hapo.
Eng. Machumu K. Machumu amewambia wakaguzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kuwa chuo cha VETA
Ndolage kikipandishwa hadhi kuwa Chuo cha Wilaya miundombinu inayokosekana lazima itawekwa ili kiweze kufikia
hadhi inayostahili kuwa kabisa chuo cha wilaya.
"Kama hiki mkishasema ni chuo cha wilaya lazima miundombinu yote inayokosekana itawekwa ili kuweza kufikia ubora
wa kuwa kabisa chuo cha wilaya, kwa mfano vyuo vingine ambavyo ni vikubwa kabisa unakuta wanatumia mifumo ya
SPJ kwa hiyo nafikiri nyinyi mkishaomba kuwa chuo cha VETA Ndolage kiwe cha wilaya basi na sisi tutakuwa na uwezo
wa kufikia hadhi kubwa kama vyuo vya vyeta vingine". ameeleza Eng. Machumu K. Machumu.
Katika ripoti yake Eng. Machumu K. Machumu ameweza kuwaeleza wakaguzi baadhi ya huduma zitolewazo Chuoni hapo
ni pamoja na mafunzo ya mda mrefu miaka miwili (2), katika fani nne (4) ambazo ni Uhazili, Uashi, Uungaji vyuma na
Teknolojia ya nguo kwa masomo ya kutwa na vilevile ameweza kueleza kuwa Chuo mafunzo kinatoa mafunzo ya mda
mfupi katika fani za Ufugaji, Kilimo, Uashi, Kompyuta, Uungaji vyuma, Uhazili na Teknolojia ya nguo.
Mbali na hayo Mkuu wa Chuo cha VETA Ndolage amesema kuwa Chuo kinatoa huduma mbalimbali nje ya mafunzo
ya kawaida kama vile kufanya shughuli za Ujenzi, Kushona sare za shule mbalimbali pamoja na kutengeneza bidhaa
za chuma kama vile mageti madirisha na milango.
Aidha, Mkuu wa Chuo cha VETA Ndolage ameweza kuongeza kwa kueleza kuwa Chuo cha VETA Ndolage pia kinatoa
mafunzo ya ziada ikiwa ni pamoja na kutengeneza Wine kwa kutumia ndizi pamoja na kutengeneza vitafunwa kama
clips zinazotokana na zao la ndizi, na kueleza kuwa mafunzo hayo hutolewa na watu wa SIDO kwa kushirikiana na
walimu wa VETA.
"Ikifika mda wa kuanzia saa nane mchana kuna watu wengi kama mia nne (400) huja chuoni hapa kwa ajiri ya kujifunza
kutengeneza Wine kwa kutumia ndizi pamoja na kutengeneza Clips kama vitafunwa vinavyotokana na zao la ndizi na
wanaotoa mafunzo ni watu wa SIDO kwa kushirikiana na walimu wa VETA na baada ya mafunzo tunategemea watu
watatengeneza vikundi ili waanze kuzalisha bidhaa zinazotokana na ndizi". amemalizia Eng. Machumu K. Machumu.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa