Katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika ndani ya ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Kupitia Taarifa ya hesabu za mwisho za Halmashauri kwa Mwaka wa fedha 2022/2023 Baraza la Madiwani limepokea na kuridhishwa na Taarifa ya Hesabu za Mwisho za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Akizungumza Katika Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mhe.Magongo Justus amewaeleza Waheshimiwa Madiwani kuwa watakwenda kujifunza namna bora ya kutambua miradi na namna bora ya kufanya tathmini ya miradi ili kuweza kuwasaidia kuwajengea uwezo mzuri wa kusimamia miradi.
"Taratibu zifanyike kusudi hawa waheshimiwa Madiwani waweze kutoka na kwenda kujifunza namna bora ya kutambua miradi na kuifanyia tathmini na tukishatoka kwenye mafunzo haya Muleba itapanda zaidi kwenye mapato kwa sababu tayari itakuwa na watu wenye uelewa na watu wenye uwezo wa kutathmini miradi " amesema Mhe. Magongo Justus.
Kwa upande wake Mhe. Reodgard Peter Chonde Diwani wa Kata ya Kamachumu ameeleza kuwa wao kama Madiwani ni lazima wawe na ujuzi katika usimamizi wa miradi na baada ya ziara ya kwenda kujifunza namna bora ya usimamizi wa miradi itawasaidia kuwa na elimu na uzoefu wa kutosha kuhusiana na namna bora ya usimamizi wa miradi.
Naye Mhe. Elton Isaya Diwani Kata Kibanga amesema kuwa hapo awali walikuwa wanapata changamoto wakati ilipokuwa ikaletwa miradi kwenye Kata zao ambayo hawana uelewa wa kutosha kuhusu miradi hiyo kwahiyo wanaamini kuwa wakijengewa uwezo itawasaidia kuleta maendeleo kwa wananchi na kukuza Halmashauri.
Imetolewa na.
Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa