Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Muleba linaloongozwa na Mhe.Magongo Justus Mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kata ya Muhutwe leo tarehe 14 Februari, 2024 limehitimisha kujadili mapendekezo ya mpango wa bajeti wa Halmashauri kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2024-2025 ambapo limeidhinisha na kupitisha rasimu ya Mpango wa bajeti ya fedha kiasi cha Tshs Bil.79,982,847,750.
Akiwasilisha Mpango wa bajeti Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu wa Halmashauri Ndug.Evart Kagaruki ameeleza kuwa katika kuandaa mpango huu wa bajeti Vipaombele mbali mbali vilizingatiwa ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara ya watumishi,kuendesha vikao vya kisheria,kutoa ruzuku ya uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari, kuimarisha Miundombinu iliyopo katika maeneo ya kutolea huduma za kijamii na kiuchumi,ukamilishaji wa Miradi viporo,ulipaji wa Madeni ya wakandarasi na watoa huduma wanaoidai Halmashauri,kuendesha mitihani ya ndani na kitaifa(Shule za Msingi na Sekondari),uboreshaji wa huduma za Afya kwa kununua madawa na vifaa tiba na kutoa elimu ya afya na usafi wa mazingira pamoja na kutekeleza miradi yenye lengo la kuongeza mapato ya Halmashauri kama vile ujenzi wa Jengo la Soko kuu la kariakoo.
Aidha,baraza la Madiwani kwa robo hii ya pili pia limepitisha rasimu ya Mpango wa bajeti ya wakala wa Barabara vijijini na mijini (TARURA) kiasi Cha Tshs Bil.4,300,923,478.
Akiwasilisha mpango wa bajeti Kaimu Meneja Mkuu wa TARURA Mhandisi Dativa K.Telesphory amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2024-2025 Halmashauri ya Wilaya ya Muleba imeidhinishiwa kiasi Cha Tshs Bil.4,300,923,478.26 kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwa kupitia vyanzo vitatu ambavyo ni kutoka mfuko wa Barabara kiasi cha Tshs Bil.1,300,923,478 Shilingi Bil.1,000,000,000 kutoka hazina(Jimbo) na kiasi Cha Tshs 2,000,000,000 kutoka hazina kama tozo ya mafuta.
Imeandaliwa na kutolewa na;
Eusebius J. Kiluwa
KAIMU MKUU KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa