Katika Baraza la Madiwani lililofanyika ndani ya Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba kujadili mapendekezo ya Mpango wa Bajeti ya mwaka 2023-2024 baraza limepitisha kiasi cha Tsh. Bilioni 71.5 kutumika katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Halmashauri katika mwaka wa fedha 2023-2024.
Akizungumza baada ya kupitisha kiasi hicho cha fedha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mhe. Magongo Justus amesema kuwa asilimia arobaini ya fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri zitaenda kutekeleza shughuli za maendeleo kwa wananchi na kiasi kingine cha fedha kitaenda kwenye matumizi ya mishahara ya watumishi wa mda pamoja na uendeshaji wa shughuli za Halmashauri.
"Sasa tumejiwekea dira inawezekana isifikie asilimia mia moja kwa sababu ndo tunaenda kutafta inawezekana tukapata asilimia mia moja au tusipate asilimia mia moja lakini angarau tuna dira ya kwamba tunataka kufikia mahali flani"
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Muleba Ndg. Greyson Mwengu amelipongeza baraza hilo kwa kuvitambua vyanzo vya mapato na kiasi cha mapato yatakayokusanywa na maeneo mapato hayo yameelekezwa ku
"Msipo kuwa na utaratibu au msipotengeneza utaratibu wa nini unachokitaka katika mwaka wa fedha unaoingia huwezi kujua unaenda kutumia nini hivyo ni lazima ujue vyanzo vyako vya mapato ni vipi na utakusanya mapato kiasi gani na utaelekeza katika maeneo yapi na suara ni suara la Kisheria ambalo Baraza hili limetekeleza kwa siku ya leo " amesema Ndg. Greyson Mwengu.
Reodigadi Peter Chonde Diwani wa Kata ya Kamachumu amesema kuwa kwa kiasi ambacho kimepitishwa kinakwenda kukidhi maeneo yote muhimu ambayo yanafaa ikiwemo miundombinu ya elimu na ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa na utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Alexander Petro Diwani wa Kata ya Bisheke amesema kuwa katika bajeti hiyo itasaidia katika ujenzi wa vyoo katika shule za Msingi ambavyo vilikuwa changamoto na kusaidia kuboresha maendeleo ya wananchi.
Katika Mwaka wa fedha 2023-2024 Halmashauri imepitisha kiasi cha Tsh. Bilioni 71.5 ambapo kiasi cha Tsh. Bilioni 64.9 zitakuwa ni fedha za ruzuku kutoka Serikali Kuu na Kiasi cha Tsh. Bilioni 6.6 kitakusanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Imetolewa na:
kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa