• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya muleba
    • Dira na Dhima
    • Core Values
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara/Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Mali asili
      • Ugavi
      • TEHEMA
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utumishi
      • Fedha
      • Mipango na Uchumi
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo/Umwagiliaji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ratiba
  • Madiwani
    • Ratiba
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Vikao vya Mhe.Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
  • Miradi
    • Itakayo- Tekelezwa
      • Inayo-Endelea
      • Iliyo-Kamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za ofisini au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Makitaba ya Picha
      • gallery

ZANA HARAMU ZA UVUVI ZAENDELEA KUTEKETEZWA MULEBA

Imewekwa : June 23rd, 2022

Zana haramu za uvuvi, zenye thamani ya Tsh. bilioni 1.25 kutoka katika Kata za mwambao wa Ziwa Victoria, Ziwa Burigi na Visiwani, zimeteketezwa eneo la mwalo wa Katunguru, uliopo kijiji Katunguru, kata ya Gwanseli, Wilaya ya Muleba.

Akizungumza kabla ya zoezi la uteketezaji wa zana hizo, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhe. Toba Nguvila ameendelea  kuwasisitiza viongozi na wananchi kuwa mstari wa mbele kupambana kutokomeza uvuvi haramu ili kuwa na uvuvi endelevu wenye manufaa katika Wilaya ya Muleba.

"Msikubali kamwe wavuvi haramu wakaendelea kuvua na timba na makokoro zana ambazo zinavua mpaka samaki wachanga tusipopambana na kuhakikisha tunawabaini wavuvi haramu na kuwachukulia hatua tutabaki na maji matupu bila samaki" amesema Mhe. Nguvila.

Aidha, amewataka wananchi kulinda ziwa na raslimali zake kama wanavyolinda mboni za macho yao kwa manufaa yao na vizazi vijavyo ambapo amewaeleza kuwa uvuvi haramu ukitokomezwa wataweza kukua kiuchumi na biashara ya samaki itakua zaidi.

"Mfanyabiashara yeyote anayewaletea nyavu haramu huyo ni muuaji mkimuona mfanyabiashara anayewaletea nyavu haramu mtoe taarifa haraka ili achukuliwe hatua za kisheria" ameendelea kueleza Mhe. Nguvila.

Sambamba na hayo amewasihi wananchi kuanzisha ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba na kuwaeleza kuwa Serikali tayari imetoa kipaumbele kwenye bajeti inayokuja kuanzisha ufugaji wa samaki kwa vizimba hivyo kuwafanya wavuvi kufuga samaki na kuendela kunufaika na uvuvi halali.

Akisoma taarifa fupi kabla ya uteketezaji wa nyavu hizo Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba Ndg. Wirfred Tibendelana amesema zoezi hili ni mwendelezo wa kutokomeza uvuvi haramu kwa wavuvi wanaotumia zana haramu kwa kuzingatia Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2020 ambazo zinamtaka mvuvi kutotumia zana haramu ikiwemo nyavu za chini ya inchi 6 katika shughuli za uvuvi.

Ndugu Agripina Joas Matungwa, mkazi wa Katunguru ameonyesha kuchukizwa na uvuvi haramu na kueleza kuwa kutokana na uvuvi haramu samaki hawapatikani kama zamani hivyo ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha uvuvi haramu unatokomezwa katika Wilaya ya Muleba.

Uchomaji wa zana hizi ni mwendelezo wa zoezi la kupambana na uvuvi haramu ambapo zana haramu zilizochomwa ni pamoja na kokoro 44, nyavu chini ya inchi 6 nyavu 11, timba 356 katuli 2 na Kamba za  kuvuta kokoro zenye urefu wa mita 810 ikiwa watuhumiwa waliokamatwa ni wavuvi 34.

Imetolewa na:

Kitengo cha Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano (W),

Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

Matangazo ya kawaida

  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA MSAIDIZI WA HESABU NAFASI MOJA November 22, 2023
  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI III NAFASI SABA November 22, 2023
  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA UDEREVA II NAFASI NNE November 22, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA SHULE ZA BWENI,UFUNDI NA SHULE MAALUM December 18, 2020
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HALMASHAURI YA MULEBA YASAINI MKATABA WA UJENZI WA SOKO LA KISASA

    January 22, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA KWA KISHINDO TAARIFA ZA HESABU ZA MWISHO ZA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    September 24, 2024
  • MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI BIL 8.1 WILAYANI MULEBA YATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU,2024.

    September 29, 2024
  • MWENGE WA UHURU MKOA WA KAGERA 2024 WAHITIMISHA MBIO ZAKE KATIKA HALAMASHAURI YA MULEBA

    September 30, 2024
  • Angalia zote

Video

Hotuba ya jana ya Rais akiwa nchini Kampala
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ajira
  • Kagera
  • Immigration

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • IKULU
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais- UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Kagabiro

    Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera

    Simu: +255 (28) 222-4013

    Simu:

    Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz

Mawasiliano mengineyo

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa