• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya muleba
    • Dira na Dhima
    • Core Values
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara/Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Mali asili
      • Ugavi
      • TEHEMA
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utumishi
      • Fedha
      • Mipango na Uchumi
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo/Umwagiliaji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ratiba
  • Madiwani
    • Ratiba
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Vikao vya Mhe.Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
  • Miradi
    • Itakayo- Tekelezwa
      • Inayo-Endelea
      • Iliyo-Kamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za ofisini au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Makitaba ya Picha
      • gallery

WATUMISHI FANYENI KAZI KWA WEREDI NA UBORA-RC MEJA JENERALI CHARLES MBUGE

Imewekwa : July 11th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge amewahimiza watumishi kufanya kazi kwa weledi mkubwa sana na viwango ili wananchi waweze kupata matunda bora ya Serikali yao.     

Ametoa kauli hiyo alipokutana na kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri na kuwaeleza kuwa wakiwajibika na kufanya kazi vizuri wananchi wataipenda na kuzidi kuiamini Serikali yao.

"Unapowajibika kwa dhati kutoka ndani ya moyo wako na kuwajibika ipasavyo hapo utakuwa umewatendea haki wananchi unawatumikia na ndipo wananchi wanavyozidi kuipenda Serikali yao na kuiamini katika kuwaletea maendeleo" amesema Meja Jenerali Charles Mbuge.

Sambamba na hayo amewahimiza watumishi kuwa na umoja na mshikamano ili kuepusha migogoro baina yao na ili waweze kufanya kazi kwa kiwango na ubora unaotakiwa katika kuwatumikia wananchi.

Taarifa iliyosomwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Ndg. Elias Kayandabila amesema kuwa Halmashauri ya wilaya ya Muleba inakusanya mapato makubwa kupitia vyanzo vitatu kutoka sekta ya uvuvi ambavyo ni tozo za leseni za uvuvi, ushuru wa mazao ya uvuvi na tozo za faini kwa makosa mbalimbali ya uvuvi yaliyokiukwa na wavuvi/wafanyabiashara wa mazao ya samaki.

Pia amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri imekusanya jumla ya Tsh. Bilioni 3.2 kati ya Tsh. Bilion 2.9 zilizokisiwa kukusanywa kupitia mazao ya uvuvi. Aidha Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022 imekusanya jumla ya mapato Tsh. bilioni 5.8 kati ya hizo Tsh. bilioni 3.2 imekusanywa kutoka kwenye  Sekta ya Uvuvi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila ameeleza kuwa kupitia mapato ya ndani Halmashauri imejenga Kituo cha Afya katika kisiwa cha Bumbile kwa kiasi cha Tsh. Milioni 500, kituo ambacho kitaenda kuwanufaisha wananchi hususani wa visiwani kwa kupata huduma za matibabu kwa urahisi kuliko kuja nchi kavu.

Lakini pia amesema kuwa katika suala la kupambana na utoroshwaji wa kahawa za magendo, Wilaya imeendelea kuwaelimisha wananchi juu ya utaratibu mpya wa kuuza kahawa kwa njia ya mnada ambao unakwenda kuwanufaisha wakulima wadogo kupitia zao hilo la Kahawa.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.

Matangazo ya kawaida

  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA MSAIDIZI WA HESABU NAFASI MOJA November 22, 2023
  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI III NAFASI SABA November 22, 2023
  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA UDEREVA II NAFASI NNE November 22, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA SHULE ZA BWENI,UFUNDI NA SHULE MAALUM December 18, 2020
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HALMASHAURI YA MULEBA YASAINI MKATABA WA UJENZI WA SOKO LA KISASA

    January 22, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA KWA KISHINDO TAARIFA ZA HESABU ZA MWISHO ZA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    September 24, 2024
  • MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI BIL 8.1 WILAYANI MULEBA YATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU,2024.

    September 29, 2024
  • MWENGE WA UHURU MKOA WA KAGERA 2024 WAHITIMISHA MBIO ZAKE KATIKA HALAMASHAURI YA MULEBA

    September 30, 2024
  • Angalia zote

Video

Hotuba ya jana ya Rais akiwa nchini Kampala
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ajira
  • Kagera
  • Immigration

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • IKULU
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais- UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Kagabiro

    Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera

    Simu: +255 (28) 222-4013

    Simu:

    Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz

Mawasiliano mengineyo

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa