• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya muleba
    • Dira na Dhima
    • Core Values
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara/Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Mali asili
      • Ugavi
      • TEHEMA
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utumishi
      • Fedha
      • Mipango na Uchumi
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo/Umwagiliaji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ratiba
  • Madiwani
    • Ratiba
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Vikao vya Mhe.Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
  • Miradi
    • Itakayo- Tekelezwa
      • Inayo-Endelea
      • Iliyo-Kamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za ofisini au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Makitaba ya Picha
      • gallery

WATOA HUDUMA ZA AFYA WAHIMIZWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WAGONJWA-DR MAGEMBE

Imewekwa : June 27th, 2022

Naibu Katibu Mkuu (Afya), Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa OR-TAMISEMI Dr. Grace Magembe amewahimiza watoa huduma za afya kuwahudumia vizuri wagonjwa kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao, heshima na utu.

Ameyaeleza haya akiwa katika ziara yake ya kukagua miundombinu ya Zahanati na Vituo vya Afya vilivyopokea fedha za miradi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 alipozungumza na watumishi wa Kituo cha Afya cha Kaigara kwa kuwasihi watoa huduma za afya kuwapokea, kuwajibu vizuri wagonjwa, kuwaelekeza kwa kuwatolea ufafanuzi mzuri kuhusiana na huduma zinazotolewa katika Vituo vya Afya na Zahanati.

"Watumishi wenzangu wa idara ya Afya, mgonjwa anapokuja kutibiwa, mjibu kwa kauli nzuri  lakini pia tuwe wepesi kutoa ufafanuzi kwa wagonjwa kuhusiana na  huduma zinazotolewa kwenye Vituo vya Afya na Zahanati,” amesema Dr. Magembe.

Dr Magembe ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la dharula katika kituo hicho na kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha anasimamia na kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo ili liweze kumalizika haraka ndani ya muda unaotakiwa.

Pia ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa katika eneo la Marahara, kata ya Magata Karutanga na kuagiza kuwepo kwa mpango kazi ambao unaonesha kila hatua ya ujenzi pamoja na  kuimarishwa kwa kasi ya usimamizi na kuongeza kasi ya ujenzi.

Na ametembelea na kukagua ujenzi wa jengo la mama na mtoto, jengo la kuhifadhia maiti, jengo la upasuaji pamoja na nyumba ya watumishi katika Kituo cha  Afya Nshamba pamoja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje  na jengo la maabara katika zahanati ya Buganguzi. 

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Evart Kagaruki  ametoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa fedha ambazo zimeletwa wilayani Muleba kutekeleza miradi ya maendeleo na kumueleza Naibu Katibu Mkuu kuwa watahakikisha wanasimamia na kutekeleza kama alivyowaelekeza ili kazi iweze kumalizika kwa wakati.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Buganguzi Mhe. Renatus Theophili Rumota amesema kuwa ujenzi wa mradi ukikamilika utaweza kusaidia upatikanaji wa huduma za uhakika katika zahanati hiyo pamoja na kusaidia  kata za Kishanda, Ijumbi, Kabilizi na Ibuga ambazo baadhi ya vijiji vyake vinapata huduma ya afya katika zahanati hiyo ya Buganguzi.

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Buganguzi Dr. Selina Sanga amemuomba Naibu Katibu Mkuu kuwaongezea watumishi katika Zahanati hiyo pale mradi utakapokamilika ili kuongeza nguvu kazi.

Imetolewa na:

Kitengo cha Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano,

Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

Matangazo ya kawaida

  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA MSAIDIZI WA HESABU NAFASI MOJA November 22, 2023
  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI III NAFASI SABA November 22, 2023
  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA UDEREVA II NAFASI NNE November 22, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA SHULE ZA BWENI,UFUNDI NA SHULE MAALUM December 18, 2020
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HALMASHAURI YA MULEBA YASAINI MKATABA WA UJENZI WA SOKO LA KISASA

    January 22, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA KWA KISHINDO TAARIFA ZA HESABU ZA MWISHO ZA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    September 24, 2024
  • MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI BIL 8.1 WILAYANI MULEBA YATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU,2024.

    September 29, 2024
  • MWENGE WA UHURU MKOA WA KAGERA 2024 WAHITIMISHA MBIO ZAKE KATIKA HALAMASHAURI YA MULEBA

    September 30, 2024
  • Angalia zote

Video

Hotuba ya jana ya Rais akiwa nchini Kampala
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ajira
  • Kagera
  • Immigration

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • IKULU
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais- UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Kagabiro

    Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera

    Simu: +255 (28) 222-4013

    Simu:

    Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz

Mawasiliano mengineyo

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa