Katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi yaliyofanyikKimkoa wilayani Muleba katika Ukumbi wa Suzana Hotel Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge amewahimiza wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa kiwango na kwa weredi.
Akizungumza maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa amesema kuwa wafanyakazi wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii,umahili na weredi kwa kasi inayohitajika ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wateja wetu.
"Sisi ni wateule wachache ambao tumebahatika kuteuliwa kufanya kazi kwa Watanzania wenzetu ni vema tusiwahi kutoka kazini tukifanya hivo tutakuwa tumetimiza wajibu wetu na kuiachia serikali yetu sikivu ili iweze kufufikilia katika masilahi na changamoto zilizopo katika maeneo yetu ya kazi" amesema Meja Jeneral Charles Mbuge.
Aidha, Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa miongoni mwa mambo yaliyofanywa na serikali katika kuboresha masilahi ya watumishi ni pamoja na kutunga sera mpya za malipo ya mishahara na motisha kwa watumishi wa umma na kuundwa kwa bodi ya mishahara katika utumishi wa umma.
Lakini pia amewambia wafanyakazi kuwa tayari serikali imeshatoa maelekezo kwa mifuko yote ya jamii kuhakikisha wafanyakazi pale wanapostaafu wanapatiwa mafao yao kwa wakati.
Sambamba na hayo ametoa wito kwa wafanyakazi wote kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kuwaeleza kuwa haki inakwenda sambamba na wajibu hivyo kila mtu anatakiwa kuhakikisha anatimiza wajibu wake kwa kufanya kazi kwa bidii maarifa na kuondoa ubinafsi ambao ni sumu kubwa kwa wafanyakazi.
Akizungumzia Mabaraza ya wafanyakazi amewaagiza waaajili wote wa Mkoa wa Kagera kuhakikisha Mabaraza yote yanakuwa hai ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa mujibu wa sheria pamoja na kukutana mala mbili kwa mwaka.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila ametoa rai kwa wafanyakazi waliotunukiwa tuzo za utendaji kazi bora kuendelea kutimiza majukumu mbalimbali ya waajili wao wanapokuwa kazini kwa kudumisha nidhamu na uchapakazi mzuri wa kazi ili kuongeza ufanisi kwenye maeneo yao ya kazi.
Imeandaliwa na Kutolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Muleba.
Kagabiro
Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera
Simu: +255 (28) 222-4013
Simu:
Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz
Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa