• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya muleba
    • Dira na Dhima
    • Core Values
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara/Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Mali asili
      • Ugavi
      • TEHEMA
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utumishi
      • Fedha
      • Mipango na Uchumi
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo/Umwagiliaji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ratiba
  • Madiwani
    • Ratiba
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Vikao vya Mhe.Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
  • Miradi
    • Itakayo- Tekelezwa
      • Inayo-Endelea
      • Iliyo-Kamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za ofisini au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Makitaba ya Picha
      • gallery

HALMASHAURI YA MULEBA YAVUKA LENGO UKUSANYAJI WA MAPATO KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

Imewekwa : August 16th, 2024

Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera imevuka lengo la makusanyo ya mapato ya ndani kwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 8.6 sawa na asilimia 125 ya lengo  kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mhe.Magongo Justus amesema hayo kwenye kikao cha baraza la Madiwani cha kujadili taarifa za robo ya nne ambacho kimefanyika agosti 16 mwaka huu katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya.

Mhe.Magongo amesema kuwa awali walikuwa wamelenga kukusanya shilingi bilioni 6.5 hivyo kutokana na ushirikiano wa Madiwani na watumishi wa Wilaya hiyo wameweza kuvuka lengo na fedha hizo zimeenda kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

“ tulipanga kukusanya  na kutumia bilioni sita na milioni mia tano  lakini tumefanikiwa kukusanya bilioni nane na point sita ambayo  ni sawa na asilimia 125 ni swala ambalo limepelekea kutekeleza miradi mbalimbali katika  ngazi zetu za kata na vijiji lakini pia kuindesha halmashauri yetu”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga   amelitaka baraza la madiwani kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kuongeza ukusanyaji wa mapato.

 Pia amewataka madiwani kusimamia swala la lishe  mashuleni ili  kuondoa hali ya udumavu kwa watoto  ikiwa ni pamoja  na kutoa elimu ya lishe kwa wazazi na  walezi.

“watoto wetu huko wanasoma kuanzia asubuhi mpaka jioni hawajapata  chakula jambo hili lazima tulikatae sote na tuseme watoto wetu, wazazi wetu huko wachangie chakula kwa watoto wetu ili wasome katika mazingira rafiki”

Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi  mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, Wakuu wa Taasisi, Kamati ya usalama ya  wilaya na viongozi wa dini.


Matangazo ya kawaida

  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA MSAIDIZI WA HESABU NAFASI MOJA November 22, 2023
  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI III NAFASI SABA November 22, 2023
  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA UDEREVA II NAFASI NNE November 22, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA SHULE ZA BWENI,UFUNDI NA SHULE MAALUM December 18, 2020
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HALMASHAURI YA MULEBA YASAINI MKATABA WA UJENZI WA SOKO LA KISASA

    January 22, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA KWA KISHINDO TAARIFA ZA HESABU ZA MWISHO ZA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    September 24, 2024
  • MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI BIL 8.1 WILAYANI MULEBA YATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU,2024.

    September 29, 2024
  • MWENGE WA UHURU MKOA WA KAGERA 2024 WAHITIMISHA MBIO ZAKE KATIKA HALAMASHAURI YA MULEBA

    September 30, 2024
  • Angalia zote

Video

Hotuba ya jana ya Rais akiwa nchini Kampala
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ajira
  • Kagera
  • Immigration

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • IKULU
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais- UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Kagabiro

    Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera

    Simu: +255 (28) 222-4013

    Simu:

    Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz

Mawasiliano mengineyo

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa