• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za wafanyakazi |
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya muleba
    • Dira na Dhima
    • Core Values
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara/Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Mali asili
      • Ugavi
      • TEHEMA
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utumishi
      • Fedha
      • Mipango na Uchumi
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo/Umwagiliaji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ratiba
  • Madiwani
    • Ratiba
      • Kuonana na Mwenyekiti
      • Vikao vya Mhe.Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
  • Miradi
    • Itakayo- Tekelezwa
      • Inayo-Endelea
      • Iliyo-Kamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za ofisini au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi mbalimbali
    • Makitaba ya Picha
      • gallery

DC NGUVILA ATEMBELEA NA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA USAMBAZAJI WA UMEME WA REA MULEBA

Imewekwa : June 22nd, 2022

Katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na idara/taasisi mbalimbali za Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila na wajumbe wa Kamati ya Usalama wa Wilaya wametembelea na kukagua utekelezaji wa usambazaji wa umeme wa REA awamu ya tatu katika vijiji vya Bweyenza, Kangoma na Nyakashenye vilivyopo kata ya Mubunda, wilaya ya Muleba.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, amemtaka Mkandarasi kumaliza kazi kwa uharaka ili wananchi waweze kupata umeme. Pia amemueleza kuwa kiu ya wananchi ni kupata umeme hivyo anatakiwa kuhakikisha anakamilisha mradi mzima kwenye vijiji vyote 30 ndani ya muda aliopewa katika mkataba pasipo kuvuka miezi sita waliyobakiza.

"Ndani ya siku 14 kwa wale wote ambao watakuwa karibu na nguzo wawashiwe umeme ili waanze kunufaika na umeme kwa sababu mmenieleza kuwa vifaa vipo, nguzo nimeziona na nyaya zipo hivyo wananchi kazi yenu ni kuunga nyaya majumbani ili wanapofika hapa wanakuwekea mita ili uendelee kuishi kwenye mwanga", amesema Mhe. Nguvila.

Aidha, amemsihi Mkandarasi kutoa taarifa kwa wananchi endapo kuna ukataji wa miti, migomba, mibuni na mazao mengine kwenye maeneo ambayo wanapitisha nguzo/kwenye njia za kupitisha nguzo ili kuepusha malalamiko kutoka kwa wananchi.

Sambamba na hayo amemtaka Mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha anawalipa vibarua stahiki zao kwa wakati huku akiwataka vibarua nao kufanya kazi kwa bidii na uaminifu ili kazi iishe kwa wakati na malengo yaliyokusudiwa yakamilike.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkandarasi wa mradi huo Mhandisi Padon Emmanuel amesema kuwa ndani ya siku 14 vijiji vya Bweyenza, Kangoma na Nyakashenye watawashiwa umeme huku akiahidi kumaliza mradi kwa vijiji vyote 30 ndani ya miezi sita kama alivyosaini katika mkataba.

Paschal Maxmilian mkazi wa kijiji cha Kangoma ameeleza kuwa kwa Serikali kuwapelekea umeme wataondokana na changamoto ya kutumia umeme wa nishati ya jua unaotegemea jua ambapo kipindi cha mvua wanapata changamoto hivyo umeme utakapowashwa wataweza kuchaji simu, kufanya shughuli za uchomeleaji na kuwa na nishati ya mwanga majumbani.

Naye Jackson Thadeo mkazi wa kijiji cha Kangoma amesema kuwa baada ya kupata umeme itawasaidia kunufaika na umeme huo kwa kueleza kuwa watafungua vibanda vya kunyolea nywele na kazi mbalimbali za kuwaingizia kipato

Imetolewa na:

Kitengo cha Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano,

Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

Matangazo ya kawaida

  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA MSAIDIZI WA HESABU NAFASI MOJA November 22, 2023
  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI III NAFASI SABA November 22, 2023
  • MATOKEO YA USAILI WA NAFASI YA UDEREVA II NAFASI NNE November 22, 2023
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA SHULE ZA BWENI,UFUNDI NA SHULE MAALUM December 18, 2020
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HALMASHAURI YA MULEBA YASAINI MKATABA WA UJENZI WA SOKO LA KISASA

    January 22, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA KWA KISHINDO TAARIFA ZA HESABU ZA MWISHO ZA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    September 24, 2024
  • MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI BIL 8.1 WILAYANI MULEBA YATEMBELEWA NA KUKAGULIWA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU,2024.

    September 29, 2024
  • MWENGE WA UHURU MKOA WA KAGERA 2024 WAHITIMISHA MBIO ZAKE KATIKA HALAMASHAURI YA MULEBA

    September 30, 2024
  • Angalia zote

Video

Hotuba ya jana ya Rais akiwa nchini Kampala
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ajira
  • Kagera
  • Immigration

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • IKULU
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Ofisi ya Rais- UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Kagabiro

    Sanduku la Barua: 131 Muleba, Kagera

    Simu: +255 (28) 222-4013

    Simu:

    Barua Pepe: ded@mulebadc.go.tz

Mawasiliano mengineyo

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimilki@2017 Haki zote zimehifadhiwa